Monday, January 13, 2020

WATAALAM NBS WAPIGWA MSASA UKUSANYAJI TAKWIMU



Mtakwimu Mkuu, Dkt.Albina Chuwa akiwa katika picha ya Pamoja na
Maafisa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kufua Warsha ya siku
mbili Jijini Dar es Salaam leo Januari 13, 2020.
Mtalaam Mwandamizi wa Takwimu kutoka Ofisi ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa, Yannis Derbali akieleza jambo kwa Mtakwimu Mkuu na maafisa kutoka
Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kufua Warsha ya siku mbili Jijini Dar es Salaam leo Januari 13, 2020.
********************************
Na. Mwandishi Wetu- MAELEZO
Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Ofisi ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa imeendesha Warsha ya Siku mbili kwa wataalamu wa
Takwimu nchini
kutoka, ili kuwezesha kuwa na utaalam na ufanisi mkubwa katika kukusanya takwimu hasa kwenye kipingele za matumizi bora ya Teknolojia mpya.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mtakwimu Mkuu, Dkt. Albina Chuwa amesema lengo la Warsha hiyo ni kuwaandaa vijana kuendena na teknolojia ya sasa katika
ukusanyaji takwimu, kwani warsha inahusisha mafunzo ya rasimu mpya ya methodolojia ya kupima kiashiria namba 17.14.1 cha Malengo ya Maendeleo endelevu cha 2030(SDGs) kilichoandaliwa na Ofisi ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa.

“Ofisi ya Mazingira ya Omoja wa Mataifa imefanya kazi kubwa kuandaa rasimu ya methodolojia ya kupima kiashiria namba 17.14.1 cha malengo ya maendeleo
endelevu, kwa hiyo kufanyika kwa warsha hii kutasaidia vijana wetu kutoka na kitu kilichobora kitakachosaidia kukusanya na kupata takwimu zilizobora na kitasaidia
kuimarisha mifumo ya kitakwimu nchini”, alisema Dkt. Albina Chuwa.

Dkt. Chuwa alisema kuwa tangu mwaka 2015, Tanzania imepiga hatua kubwa katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo endelevu ya 2030, ikiwemo kufanya
mikutano ya kutoa uelewa kuhusu SDGs na kufanya kongamano la kujenga uwezo kwa mamlaka zote za Serikali za Mitaa kuhusu SDGs na namna bora ya Kutekeleza.

Aidha Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeongeza ubunifu katika kuimarisha ushirikiano ambao unajumuisha kwa karibu wadau katika kuboresha ikolojia ya takwimu nchini
kwa ajili ya kusaidia ugatuaji wa SDGs katika ngazi za kitaifa juhudi hizi zinalenga kujenga msingi madhubuti wa upatikanaji wa Takwimu kwa ajili ya kusaidia
upangaji na ufuatiliaji mipango ya maendeleo yakitaifa na kimataifa.

Warsha hiyo ya siku mbili kwa wataalamu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu inalenga kuimarisha uelewa na teknolojia kwenye ukusanyaji takwimu ili kuweza
kuendana Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030.

Aliongeza kuwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, inashirikiana na asasi mbalimbali za kiraia ili kuwezesha kuwepo kwa uimara wa takwimu kwa ajili ya matumizi
mbalimbali ikiwemo kwenye masuala ya elimu, Uchumi, Afya, kilimo na sekta zingine za maendeleo nchini.

“Ofisi ya Taifa ya Takwimu inafanya kazi na Ofisi ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa katika kufanya majaribio yay a rasmu ya methodolojia ya kupima kiashiria
namba 17.14.1 cha SDGs 2030 ambacho kinafuatilia Idadi ya nchi zenye mifumo ya kuimarisha Mahusiano ya kisera kwa ajili ya mpango wa maendeleo endelevu kwa
hiyo Warsha hii itakuwa na manufaa makubwa kwa NBS”, alisema Dkt. Chuwa.

No comments :

Post a Comment