********************************
Na Silvia Mchuruza.
Bukoba,Kagera.
Taasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Kagera inawashikilia watumishi
wawili madaktari na mmoja wao akiwa ni daktari wa kujisomea yaani PHD
kwa
kile kilichodaiwa kuwa ni kujihusisha na vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya ofisi za umma.
kile kilichodaiwa kuwa ni kujihusisha na vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya ofisi za umma.
Akizungumza na
waandishi Wa habari katika ofisi za TAKUKURU mkoa Mkuu Wa TAKUKURU
Ndg.John K.E Joseph amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika
nyakati tofauti na kupitia wilaya tofauti za mkoa Wa kagera ambapo
amewataj majina yao madaktari hao
“Ndugu wanahabari
nichukue nafasi hii kutoa taarifa ya utendaji kazi Wa taasisi ya
takukuru toka Julai mosi mwaka 2019 hadi January 2020 ambapo tumefanya
kazi nyingi sana lakini tumebahatika kuwatia mbaloni watumishi watatu
ambapo wawili in madaktari Wa binadamu akiwemo Dr.Gresmus Gregery
Nkrunzinza ambae ni mganga Mkuu Wa hospital teule ya wilaya ya
biharamulo ambapo ameshitakiwa kwa kosa LA uchepushaji Wa dawa za mradi
Wa akina mama wajawazito na wanaojifungua kwa kuziamisha na kupeleka
kwenye duka binafsi la dawa na kuziuza pamoja”alisema Mkuu Wa takukuru
Aidha ameongeza kuwa
daktari mwingine ambae pia nae ni daktari wa binadamu Dr.Gervas Dramas
Maneto ambae anashikiliwa kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi na wizi
akiwa mtumishi Wa ummba ambapo nae ni mwajiriliwa katika hospitality
teule ya wilaya ya biharamulo.
” Daktari huyu kwa
kutambua yeye ni mtumishi Wa umma na mwajiliwa Wa serikali toka mwaka
2006 lakini mwaka 2011 alidiliki kuomba ajira nyingine katika
halmashauri ya ya jiji la mwanza na akapangiwa katika kiruo cha hospital
ya Butihama na akawa analipwa mshahara mpaka mwaka 2014 January jambo
ambalo ni kinyume cha sheria” alisema Ndg.John K.E. Joseph.
Sambamba na hayo Mkuu
Wa takukuru mkoa Wa kagera amesema kuwa katika kipindi hiki imemfikisha
mahakamani Prof. Philemon Nyangi Wambura kwa makosa ya kuomba na
kupokea rushes kutoka kwa wateja akiokuwa akiwashughulikia kikazi wakati
akiwa kaimu Mkuu Wa kampuni ya Ranchi za taiga (NARCO).
No comments :
Post a Comment