Na Silvia Mchuruza.
Kagera.
Zaidi ya Miradi
mbalimbali ya kimaendeleo imeendelea kutekelezwa katika kata ya Ruzinga
iliyopo Wilayani Missenyi Mkoani Kagera ikiwa ni kuazimisha miaka 14 ya
uchangiaji maendeleo katika kata hiyo.
Miradi hiyo ni kama
bweni la kulala wanafunzi, vyumba vya mahabara,ukarabati wa madarasa,
mfumo wa computa, sekta ya maji pamoja na afya.
Hayo yamebainishwa na
Kaimu mwenyekiti wa tamasha hilo linalofahamika kama Ruzinga
Development {Ruzinga day} bwana Paschael Kamala wakati akiongea na
halaiki ya watu waliofika kwa lengo la kushuhudia tamashahilo.
Bwana Kamala
ameongeza kuwa zaidi ya shilingi milioni 20 zimechangwa katika tamasha
la kila mwaka kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya Kata Ruzinga iliyopo
Wilayani Missenyi Mkoani Kagera.
Bwana Kamala amesema
kuwa pesa hizo zitatumika kwa ajili ya kuendelea kuchochea maendeleo ya
kata ikiwemo miundombinu ya barabara, maji, elimu, pamoja na afya uku
akiendelea kuomba msaada katika halmashauri ya Wilaya ya Missenyi na
Tanzania kwa ujumla kuunga mkono jitihada za wadau hao ambao wana uchu
wa kuona kata hiyo inapiga hatua kubwa kwenye sekta ya maendeleo .
Pamoja na michango
hiyo wadau mbali mbali wa Ruzinga day wametembelea miradi kadhaa ili
kujionea hali halisi ikiwemo kukagua shule ya sekondari Ruzinga,kituo
cha afya Ruzinga pamoja na shule ya msingi Ruhija huku wadau hao
wakishuhudia uchakavu mkubwa wa baadhi ya majengo ya shule ya msingi
Ruhija ambapo wameomba uongozi wa wilaya ya Missenyi kushirikiana nao
kufanya marekebisho.
Kwa upande wake mgeni
rasmi katika tamasha hilo ambaye ni mkurugenzi wa harmashauri ya
wilaya ya Missenyi bwana Innosent Mkandala amesifu juhudi kubwa
zinazofanywa na wadau hao wa maendeleo katika kata hiyo na kueleza kuwa
serikali itaendelea kushirikiana nao huku akiwaasa wazazi kuhakikisha
wanawapelea shule wanafunzi waliochaguliwa kijiunga na kidato cha kwanza
mwaka huu.
Katika hatua nyingine
bwana Mkandara amewapongeza wadau hao wa maendeleo katika kata hiyo
kwa kuonesha jitihada kubwa za kuinua maendeleo ya kata hiyo huku
akitaja bweni la kulala wanafunzi wa kike ambalo limejengwa kwa jitihada
kubwa za wadau hao wa maendeleo pamoja na serikali na kusema kuwa kata
hiyo ya Ruzinga ni moja kati ya kata zinazozidi kupiga hatua kubwa za
kimaendeleo na kuwa mfano wa kuigwa Wilayani Missenyi.
Kwa upande wake
Diwani wa Kata hiyo Mh Leonidas Rutagwelela ameipongeza halmashauri ya
Wilaya ya Missenyi kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikipelekwa
katika kata hiyo pindi wanapoitaji msaada wa halmashauri hiyo na
kuongeza kuwa wamekuwa wakiwa unga mkono mara kwa mara.
No comments :
Post a Comment