Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu
wa Rais, Bi Emma Lyimo (kulia) akikabidhiana nyaraka na Meneja Mkuu wa
Mgodi wa North Mara, Luiz Correia mara baada ya kushuhudia utiaji saini
wa mkataba baina ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC) na mgodi huo kwa ajili ya utekelezaji wa maagizo ya Serikali
kuhusu uzingatiaji wa Sheria za nchi ikiwemo Sheria ya Usimamizi wa
Mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake katika utekelezaji wa shughuli za
migodi. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 13, 2020 katika Ofisi za
Makamu wa Rais jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa
la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka
(kushoto) akikabidhiana nyaraka na Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara,
Luiz Correia baada ya utiaji saini wa mkataba baina ya NEMC na mgodi huo
kwa ajili ya utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhusu uzingatiaji wa
Sheria za nchi ikiwemo Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na
kanuni zake katika utekelezaji wa shughuli za migodi.
Wajumbe kutoka Mgodi wa North Mara
na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
wakipitia nyaraka kabla ya kutiliana saini kwa mkataba baina yao kwa
ajili ya utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhusu uzingatiaji wa Sheria
za nchi ikiwemo Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na
kanuni zake katika utekelezaji wa shughuli za migodi.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa
la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka
akisaini mkataba kwa ajili ya utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhusu
uzingatiaji wa Sheria za nchi ikiwemo Sheria ya Usimamizi wa Mazingira
ya mwaka 2004 na kanuni zake katika utekelezaji wa shughuli za migodi.
Mkuu wa Kitengo cha Mazingira
kutoka Mgodi wa North Mara, Bw. Tunzo Msuya akisaini mkataba wa baina
yao kwa ajili ya utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhusu uzingatiaji
wa Sheria za nchi ikiwemo Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004
na kanuni zake katika utekelezaji wa shughuli za migodi.
No comments :
Post a Comment