Monday, January 13, 2020

RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN MGENI RASMI TAARAB YA MAADHIMISHO YA MIAKA 56 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR UKUMBI WA SHEIKH IDRISA ABDULWAKIL KIKWAJUNI



KATIBU Mkuu Wizara ya Vijana Michezo Sanaa na Utamaduni Zanzibar.Ndg. Omar Hassan (King) akisoma utaratibu wa hafla ya Taarab Rasmin ya Kikundi cha Taifa kuadhimisha Sherehe za Maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh. Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsalimia Msanii Mkongwe wa Taarab Visiwani Zanzibar Bi.Mwanajuma Ali Hassan, aliyeimba wimbo wa  ( Mpunga Kinuni ) baada ya kutambulishwa wakati wa Taarab rasmin ya kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, iliofanyika kaja usiku.
MKE wa Rais wa Zanzibar.Mama Mwanamwema Shein, akimtunza muimbaji wa wa wimbo wa “ Tarehe Kumi na Moja “ Msanii Iddi Suwed, wakati wa hafla ya Taarab rasmin ya kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar jana usiku 12-1-2020.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na Mama Fatma Karume wakifuatilia moja ya wimbo ukiimbwa wakati wa hafla ya Taarab Rasmin ya kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na (kushoto kwa Mama) Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Mhe. Samia Suluhu Hassan na (kuli) Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi, wakifuatilia hafla ya Taarab Rasmnin ya Kikundi cha Taifa Zanzibar, kuadhimisha sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar
MSANII wa Kikundi cha Taifa Zanzibar. Ndg. Khamis Nyange (Profesa Gogo) akiimba wimbo wa  “Tumbili hafugiki “  wakati wa hafla ya kuadhimisha sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakili Kikwajuni Jijini Zanzibar
MSANII Mkongwe Zanzibar wa Taarab.Bi. Fatma Issa akiimba “Wimbo wa Haya Maumbile Yangu “ wakati wa hafla ya Taarab Rasmin ya Kikundi cha Taifa Zanzibar, kuadhimisha sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi Zanzibar, iliofanyika jana usiku 12-1-2020, katika ukumbi wa Sheikh. Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, mgeni Rasmin katika Taarab Maalum ya Kikundi cha Taifa Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, akijumuika na Wananchi na Viongozi, (kushoto kwa Rais) Waziri wa Vijana Michezo Utamaduni na Sanaa Zanzibar.Mhe. Balozi Ali Karume na (kulia kwa Rais) Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.
MSANII wa Kikundi cha Taifa Zanzibar,.Bi. Saada Mohammed akiimba wimbo wa “Anaetoa ni Mola “ wakati wa hafla ya kuadhuimisha sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

No comments :

Post a Comment