*****************************
Na Silvia Mchuruza.
Bukoba.
Matokeo ya Kidato cha
Nne 2019 yaliyotangazwa mnamo tarehe 09, Januari 2020, na Baraza la
Mitihani Tanzania, yameendelea kusisimu wadau mbalimbali wa Elimu
kufuatia baadhi ya Wahitimu kuonesha maajabu katika ufaulu wao.
Miongoni mwa maajabu
na rekodi iliyojitokeza katika matokeo hayo, ni pamoja na waliokuwa
Wanafunzi sita wa Shule ya Seminari ya Katoro iliyopo Mkoani Kagera,
kufaulu kwa alama nzuri sana katika matokeo ya Mtihani huo wa kuhitimu
kidato cha nne mwaka jana.
Hali hiyo imeonekana
kuwashangaza walio wengi kwani si jambo rahisi sana Kwa hofu ya mtihani
inavyokuwa, lakini watuhumiwa hawa wameweza kufanya vizuri baada ya
kuomba nafasi hiyo Kwa mamlaka zinazohusika na kesi yao, mpaka sasa
upepelezi wa kesi yao haujakamilika licha ya kuonekana wazi dalili za
uonevu kulingana na mlolongo wa kesi yao ulivyo.
Wanafunzi hao ambao
mpaka sasa wapo mahabusu Kwa kushikiliwa Kwa Tuhuma za kifo cha
Mwanafunzi mwenzao kilichotokea miezi kadhaa iliyopita, wametambulika
Kwa majina yao na ufaulu katika mabano kuwa ni Sharifu Amri (Division
II.19), Fahad Abdul-Azizi (Division II.21), Hussein Mussa (Division
II.21), Sharifu Uledi (Division II.21), Abdallah Ntarambe (Division
III.23), na Usama Ramadhani (Division III.25).
No comments :
Post a Comment