Friday, January 10, 2020

MBUNGE WA KIBAHA VIJIJINI MHE. HAMOUD ABUU JUMAA ATEMBELEA KIWANDA CHA TAN CHOICE



***************************************
Leo Jan 10 Mhe. Mbunge wa Kibaha Vijijini ametembelea Kiwanda cha TAN CHOICE kilichopo katika Kata ya Soga Halmashauri ya Kibaha Vijijini katika ziara hiyo Mhe. Mbunge aliambatana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini ndugu Lemmy Ludovick pamoja na Diwani wa Kata ya Soga ndugu Ramadhani Kilongola.
Mhe. Mbunge ameupongeza uongozi wa Kiwanda cha TAN CHOICE kwa kujenga kiwanda
hicho katika Halmashauri ya Kibaha Vijijini.
“Kiwanda hichi kitakuwa na uwezo wa kuchinja Ng’ombe 1000 na Mbuzi 5000 kwa siku ni Kiwanda kikubwa sana katika Mkoa wetu wa Pwani na Nchi yetu.” Amesema Mhe. Mbunge
Sambaba na hilo Mhe. Hamoud amefikisha salama za Mhe. Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Kassim ambaye alikuwa na ziara ya kutembelea kiwanda hicho cha TAN CHOICE.
“Mhe. Waziri Mkuu amenituma niwafikishie salama ya kuhairisha ziara yake ya leo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake lakini nia yake ipo pale pale atakuja.” amesema Mhe. Mbunge
Mwisho Mhe. Mbunge aliweza kukagua Mradi wa Maji unatoka Kongowe kuelekea Soga katika Kiwanda cha TAN CHOICE.

No comments :

Post a Comment