Wananchi wa jiji la
Arusha wakiwa wamepanga foleni kwa ajili ya kupata Namba ya Nida ili
kuweza kusajili laini zao za simu ,kufuatia zoezi la pamoja la usajili
Wa namba za simu kwa alama za vidole ambalo limeratibiwa na Mkuu Wa mkoa
Mara kufuatia agizo la mh Raid John Magufuli kusogeza mbele zoezi la
kusajili namba za simu kwa alama za vidole (picha na Happy Lazaro
Arusha.
*******************************
Happy Lazaro,Arusha.
Wananchi wa mkoa wa
Arusha wamemshukuru Rais John Magufuli kitendo cha kuwaongezea muda wa
kusajili laini zao za simu kwani asilimia kubwa ya wananchi bado
hawajasajili laini.
Wakiongea wakati
zoezi la kujiandikisha na kusajili namba zao za Nida linaloendelea
katika viwanja vya kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid walisema kuwa
asilimia kubwa ya wananchi hawajasajili laini zao kwa alama za vidole
kutokana na kutokuwa na namba za Nida .
“Foleni hii kubwa sio
kusajili kwa alama za vidole apana foleni hii imetokana na wananchi
wengi hatuna namba za Nida ,kama Mimi nimejiandikisha tangu mwaka Jana
zoezi lilivyoanza lakini hadi Leo sijapata namba wala kitambulisho
nimekuja mara kibao mara niambiwe sionekani kwenye taarifa zao za Nida
,muda mwingine unakuta picha lakini huoni namba ” alisema Steven John
Walitumia muda huo
kuomba Nida kuongeza wafanyakazi pamoja na vitendea Kazi ili zoezi
liweze kwenda kwa haraka huku wakiwasisitiza kufungua mapema vituo vyao
vya kuangalia namba za vitambulisho pamoja na kujisajili .
“Leo wengine tumekuja
saa kumi na moja usiku ,wengine Saa moja tumekaa hapa Nida wamekuja
kufungua saa tatu jamani kweli tunaomba wawahi basi kufungua ili watu
waweze kufungua haraka na kiurahisi maana watu ni wengi sana na
ikiwezekana muda wa kazi uongezwe tunaomba ili tupate huduma”Gloria
Oktavina.
Akiongea na wananchi
hao katika zoezi hilo, Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewapongeza
wananchi kwa namna ambavyo wamejitokeza kujiandikisha na kusajili namba
zao kwa uvumilivu , alisema kuwa serikali imejipanga vyema kuhakikisha
zoezi hili linaenda vyema kwa usawa .
“Viongozi wote wa
halmashauri zote za mkoa wa Arusha watasimama imara kuhakikisha zoezi
hili limekamilika ,tumegundua wananchi wengi walijiandikisha na
hawajapata vitambulisho wala namba ila wanahakikisha watafanya Kazi
usiku na mchana wanapata namba na zoezi limeisha salama” amesema Gambo.
Amesema katika
kuhakikisha Zoezi linaenda linaisha haraka wataongeza eafanyakazi Wa
Nida ambapo alisema watatumia vijana Wa JKT ili kuweza kukamilisha zoezi
hili.
Naye meneja wa
mawasiliano Kanda ya kaskazini (TCRA)Mhandisi Imelda Salim amesema
kuwa, kufuatia zoezi la pamoja la usajili wa namba za simu kwa alama
za vidole ambalo limeratibiwa na Mkuu wa mkoa kufuatia agizo la Rais
John Magufuli kusogeza mbele zoezi la kusajili namba za simu kwa alama
za vidole waliamua kusogeza kwa ukaribu zaidi huduma hii.
Amesema kuwa, wao
kama TCRA kwa kushirikiana na taasisi zingine za Nida pamoja na
makampuni ya simu wamekubaliana kushirikiana ili kukamilisha maelekezo
yaliyotolewa na Rais ,ambapo amesema kuwa zoezi hili limeanza katika
halmashauri ya jiji la Arusha na wataendeleza katika halmashauri zote
ili kila mwananchi ambae ajajiandikisha waweze kujiandikisha na kusajili
namba yake ya simu.
Amebainisha kuwa,
kuna changamoto ambayo imejitokeza kwa wananchi wengine wakienda
kujisajili laini zao kwa alama za vidole wanakuta vidole vyao
havimechi sasa tumetoa maagizo iwapo mwananchi wakienda tatizo hili
likimkuta aache taarifa zake apo na namba ya simu mtoa huduma atapeleka
hizo taarifa Nida na zitafanyiwa Kazi na tutampigia kumpa mrejesho.
No comments :
Post a Comment