
********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Shirika la reli Tanzania (TRC) limewataka wananchi, madereva wa
magari na watu wanaoishi kando kando ya reli kuzingatia usalama wa reli
ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitendo vya
uharibifu wa miundombinu.
Akizungumza wakati qa uzinduzi wa kampeni ya usalama katika
reli, Kaimu mkurugenzi wa TRC, Bw. FOCUS SAHANI amesema kuwa ili
kuimarisha usalama katika reli inapaswa kila mwananchi na wadau binafsi
kutoa taarifa za vitendo vya hujuma hizo polisi na kuhakikisha wahujumu
hao wanachukuliwa hatu za kisheria.
“Mara kadhaa kumekuwa na
matukio ya baadhi wananchi wasio raia wema wanajaribu kuiba ama kufanya
hujuma kwa kutega vyuma relini.Serikali inatambua katika maeneo hayo
wanakojaribu kuhujumu ama kutega treni,wapo raia wema”. Amesema
Bw.Sahani.
Kaimu kamishina wa jeshi la polisi kikosi cha usalama wa reli
Stanley kulyamo amesema kumekuwa kikosi hicho tayari kinawashikilia watu
kadhaa kutokana na makosa ya uharibifu wa miundombinu ya reli na
uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazowakabiri.
Nae Mwanasheria wa TRC VERONICA SUDAI amesema adhabu ya kuhujumu
miundombinu ya reli ni pamoja na faini isiyopungua Milioni 50, ama
kifungo kisichopungua miaka 3.
Mkuu wa usalama wa reli Mahizo
martini mgezi amesema Madhara ya ajali za treni ni makubwa kutokana na
kubeba watu wengi kwa wakati mmoja hivyo kuwahimoza wananchi kujiepushe
na wizi wa mataruma na hujuma nyinge ili kuhakikisha usalama wa reli na
treni unakuwepo.
No comments :
Post a Comment