
*********************************
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.
Paul Makonda anawaalika wananchi wote wa Mkoa huo wenye Kero za
kisheria kujitokeza kwa Wingi kwenye Maadhimisho ya Wiki ya
Mahakama
yanayotaraji kuanza February 01 hadi 05 kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja.
RC Makonda kwa kushirikiana na
Mahakama kuu ya Kanda ya Dar es salaam wameandaa wataalamu wakiwemo
Mawakili, Wanasheria, Jeshi la polisi Dawati la Jinsia, Jeshi la
Magereza, Chama cha Wanasheria Tanganyika pamoja na wadau wa kisheria wa
kutosha kuhakikisha kila mwananchi anaefika kwenye viwanja hivyo
anapata huduma stahiki ya kisheria pasipo usumbufu wowote.
Maadhimisho ya Wiki ya Mahakama
yatatanguliwa na Maandamano yatakayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Mhe. Paul Makonda kuanzia Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam
hadi viwanja vya Mmoja mapema Asubuhi.
Walengwa wa Zoezi hilo ni Wananchi
wenye kero za migogoro iliyopo Mahakamani, Mienendo ya kesi, Wale ambao
hukumu zao zimetoka na wanataka kukata rufaa lakini hawapewi nakala za
hukumu kwa maandishi, Wananchi wasiojua wapeleke wapi kesi zao,
Malalamiko ya maabusu, Polisi pamoja na kesi za ukatili wa kijinsia.
No comments :
Post a Comment