Kaimu mkurugenzi mkuu wa TMDA, Adam Fimbo (wa tatu kushoto) akipatiwa
maelezo na watalaam wa ukaguzi wa viwanda katika moja ya kiwanda
kinachojengwa.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa TMDA, Adam Fimbo (katikati) akiwa katika picha
ya pamoja kwenye moja ya viwanda walivyotembelea katika ukaguzi.
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA), imefanya ziara ya kutembelea na
ukaguzi wa viwanda 8 vya dawa za binadamu na mifugo vinavyoendelea
kujengwa katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo
aliambatana na wakaguzi wa viwanda kuangalia hatua zilizofikiwa katika
ujenzi na kuendelea kutoa ushauri wa kitaalam ili kuwezesha viwanda
hivyo kukidhi matakwa ya kisheria katika utengenezaji sahihi wa dawa
(GMP).
Ziara hiyo ya siku tatu iliyoanza Januari 27-29 mwaka huu, ni katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano.
Viwanda vilivyotembelewa ni:-
Vista Pharmaceuticals Ltd na Kariuki Pharmaceuticals vilivyopo Zegereni,
Kibaha, Hester Biosciences Africa Ltd na Biotec Pharmaceuticals vya
mifugo vilivyopo Kibaha, Emedics Pharmaceuticals kilichopo Kerege
Bagamoyo.
Pia Cure Pharmaceuticals Ltd kilichopo Kimbiji, Kigamboni, African
Pharmaceuticals kilichopo Kisemvule Mkuranga na Alpha Pharmaceuticals
Ltd kilichopo Mbangala Rangi tatu, Temeke.



No comments :
Post a Comment