Wabunge
wa bunge la Umoja wa Ulaya wamepitisha kwa wingi sheria inayoruhusu
Uingereza kuondoka kwenye Umoja huo ama Brexit, wiki hii na kuondoa
kizingiti kikubwa cha mwisho kabla Brexit yenyewe kufanyika.
Bunge hilo limepiga kura ya kuyapitisha makubaliano ya Brexit kwa kura 621 dhidi ya 49 ambao walipinga.
Kulitakiwa wingi mdogo wa kura kwenye bunge hilo lenye wabunge 75.
Nchi wanachama hivi sasa wanatakiwa kutoa idhini ya mwisho kwenye makubaliano hayo kupitia utaratibu wa maandishi.
Uingereza
inataraji kuondoka Umoja wa Ulaya usiku wa kuamkia Ijumaa, baada ya
miaka mitatu tangu Waingereza walipoanzisha mchakato wa kuondoka ama
kusalia kwenye Umoja huo, katika kura ya maoni ya mwaka 2016.

No comments :
Post a Comment