Virusi
hivyo tayari vimeshawaua watu zaidi ya 160 na zaidi ya watu 7, 711
wameambukizwa tangu kulipotambuliwa mgonjwa wa kwanza katika jiji la
Wuhan nchini China, Disemba 31.
Mkurugenzi
mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Gebreyesus, aliyerejea kutoka China amesema
ilikuwa ni muhimu kuitisha mkutano mwingine, ambao ni wa tatu kwa wiki
hii kwa kuwa virusi hivyo vimekwishasambaa hadi nje ya China, akisema ni
hali inayozidi kutia wasiwasi.
Nchi
wanachama wa timu hiyo ya WHO iliamua wiki iliyopita kwamba janga hilo
lilikuwa bado halijafikia kiwango cha kutangazwa dharura ya dunia.
Hatua kama hiyo ilitangazwa na WHO wakati wa mripuko wa Ebola na mafua ya ndege.

No comments :
Post a Comment