Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma
Wandishi wa habari wakifuatilia mkutano wao na Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga jijini Dodoma
Kaimu Mrajisi wa Vyama vya
Ushirika nchini, Dk Benson Ndiegi akizungumza na wandishi wa habari
kwenye mkutano wa Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga jijini Dodoma.
……………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Kati ya vyama
hivyo, 2,532 sawa na asilimia 73.8 ni vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS)
ambavyo vilianzishwa wakati serikali ilipoanzisha Mfumo wa Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi (JK Fund).
Akitoa rai hiyo
jijini Dodoma Waziri wa Kilimo Mhe.Japhet Hasunga, amesema uamuzi huo
utachukuliwa baada ya siku 90, tangu Mrajis wa Vyama Vya Ushirika kutoa
tangazo kwenye gazeti la serikali.
“Vyama vingi ni
matokeo ya mfumo wa uwezeshaji wananchi kiuchumi ujulikanao kama (JK
Fund), ambao ulilenga kuwawezesha wananchi kiuchumi. Katika mpango huo
wananchi walianzisha SACCOS kwa lengo la kupata mikopo kutoka kwenye
mfuko huo,’ amesema.
Ameeleza sababu
za kuchukua uamuzi huo ni vyama kutokuwa na ofisi tangu vilipoanzishwa,
havijulikani vilipo wala viongozi wake, kutotayarisha taarifa za mapato
na matumizi, kutofunga mahesabu na kufanyiwa ukaguzi pamoja na
kutoitisha mkutano mkuu wa mwaka.
“Ninamuagiza
mrajis wa vyama vya ushirika kutangaza kusudio la kuvifuta vyama 3,436
ambavyo havitekelezi majukumu yake ya msingi na havijulikani vilipo.
Asilimia 78 ya vyama hivyo ni vya Akiba na Mikopo (SACCOS),” amesema
Mhe.Hasunga
Mhe.Hasunga amesema vipo vyama vingine 1,250 vya ushirika vilivyosinzia huku vyama 6,463 ndivyo vilivyokuwa hai.
Mchanganuo wa
vyama hivyo vinavyotarajiwa kufutwa ni SACCOS (2,537), vyama vya msingi
vya wakulima- AMCOS (264), mifugo (82), walaji (25), huduma (72),
ufugaji nyuki (17) na nyumba (8).
Vingine ni madini (23), viwanda (102), uvuvi (37), umwagiliaji (31), vyama vikuu (3) na vyama vinginevyo (235).
Ameitaja mikoa
iliyoongoza kuwa na vyama hewa vya ushirika ni Mwanza (393) Pwani (335),
Kagera (301), Morogoro (298), Arusha (282), Tabora (282) na Kigoma
(207).
Kwa upande wake
Naibu Mrajis wa Vyama Vya Ushirika nchini, Dk. Benson Ndiege, amesema
hatua zinaendelea kuchukuliwa kwa viongozi waliotafuna mali za ushirika.
Katika hatua
nyingine, Waziri Hasunga alitangaza kuwa Kamati ya Taifa ya Mbegu (NSC)
imepitisha matumizi ya aina mpya 40 za mbegu bora zilizopendekezwa na
Kamati ya Taifa ya Kupitisha Aina za Mbegu Mpya (NVRC).
Amesema kuwa
mbegu hizo mpya aina 10 ni za mahindi, 2 za mpunga, 1 ya ulezi, 3 za
pamba, 9 za muhogo, 9 za alizeti na mbegu sita za viazi vitamu.
Kwa mujibu wa
waziri huyo amesema mbegu hizo mpya zitaanza kuzalishwa na kutumika
nchini kuanzia msimu wa 2019/20, kwa mujibu wa Sheria ya Mbegu.



No comments :
Post a Comment