Baadhi ya Washiriki wa Mjadala
kuhusu Ukuaji wa Miji na Changamoto zake wakifuatilia hotuba ya Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Nicolaus
Benjamin (Hayupo pichani) wakati akifungua Mjadala huo jijini Dodoma Leo
Tarehe 30 Januari 2020. Mjadala huo umeandaliwa kwa pamoja na Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Makazi (UN Habitat).
Mkurugenzi wa
Mipango Miji na Vijiji Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Emaculata Senje akichangia katika Mjadala Kuhusu Ukuaji Miji na
Changamoto zake uliofanyika leo tarehe 30 Januari 2020 jijini Dodoma.
Mjadala huo umeandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Makazi (UN Habitat).
Washiriki wakifuatilia
uwasilishwaji Mada kwenye Mjadala kuhusu Ukuaji wa Miji na Changamoto
zake uliofanyika jijini Dodoma Leo Tarehe 30 Januari 2020. Mjadala huo
umeandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Makazi (UN Habitat).

Washiriki wa Mjadala kuhusu Ukuaji
wa Miji na Changamoto zake uliofanyika jijini Dodoma Leo Tarehe 30
Januari 2020 wakiwa katika picha ya pamoja. Aliyekaa katikati ni Kaimu
Mkurugenzi wa Mipango Miji Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Amulike Mahenge. Mjadala huo umeandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Makazi (UN Habitat). (PICHA ZOTE NA HASSAN MABUYE
WIZARA YA ARDHI)
…………………………………………………………………………………….
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Imeelezwa
kukosekana kwa sera maalum ya uendelezaji Miji nchini kunachangia
kuendelea
kuwepo makazi holela kwenye maeneo mablimbali nchini Tanzania.
Hayo yameelezwa
na Mkurugenzi wa Undelezaji Miji na Vijiji Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt Mukuka Hante leo tarehe 30 Januari
2020 wakati wa Kusanyiko la Mjadala kuhusu Masuala ya Ukuaji Miji na
Changamoto zake lililofanyika jijini Dodoma.
Alisema, kwa sasa
nchi nyingi duniani zina sera maalum ya uendelezaji miji aliyoieleza
kuwa inawezesha kuwepo chombo cha kuleta maendeleo ya miji unaoenda
sambamba na huduma za afya, makazi, barabara na huduma nyingine za
kijamii.
Hata hivyo, Hante
alisema Serikali iko mbioni kuja na sera ya Uendelezaji Miji
aliyoieleza kuwa itakuwa suluhisho la makazi holela hasa kipindi hiki
ambacho miji mingi imeendelea kukuwa kwa kasi.
Kwa mujibu wa
Hante, Uendelezaji Miji maeneo mbalimbali unatakiwa usiwe kwenye
uboreshaji makazi pekee bali uendane na mjumuiko wa uendelezaji miji na
vijiji kwa kuwa maeneo ya vijiji yanatakiwa pia kuwa na makazi bora
yatakayochangia uwekezaji. Aidha, alisema Miji na Vijiji vinategemeana
na iwapo vijiji vitaachwe kujumishwa kwenye mpango wa uendelezaji miji
basi vitaachwa mbali na wananchi wake kuwa nyuma kimaendeleo.
Mkurugenzi huyo
wa Uendelezaji Miji na Vijiji TAMISEMI alibainisha kuwa, ukuaji miji
unatoa fursa ya uwekezeji kwa wananchi vijijni na kubainisha kuwa pamoja
na mkazo kuwekwa katika uendelezaji miji lakini huduma nyingine kama
vile Afya na barabara lazima ziendelezwe hasa kipindi hiki ambacho
Seriali inapoelekea katika uchumi wa kati.
Kwa upande wake
Meya wa Jiji la Dodoma Profesa Davis Mwanfupe alisema ukuaji Miji kwenye
maeneo mbalimbali lazima uendane na upatikanaji huduma muhimu kwa lengo
la kukabiliana na changamoto na fursa zitakazopatikana. Alibainisha
kuwa, mjadala unaoendelea kuhusiana na ukuaji miji unakuja wakati
muafaka ambapo dunia iko hatua ya kujadili maendeleo endelevu kwenye
maeneo mbalimbali.
Akifungua Mjadala
huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Nicolaus
Benjamin aliwaambia washiriki wa Mjdala huo kuwa serikali ya Tanzania
imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha inapunguza ama kuondoa
makazi holela.
Hata hivyo,
aliwataka washiriki hao kuutumia mjadala huo wa siku moja kutafuta
ufumbuzi wa changamoto za makazi holela sambamba na kuibuka mpango
utakaotoa fursa za uwekezaji hasa uendelezaji miji, uratibu na
ushirikiano kati ya wadau katika kufikia lengo.
Naye Kaimu
Mkurugenzi wa Mipango Miji Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Amulike Mahenge alisema, kusanyiko la Mjadala kuhusu ukuaji Miji na
changamoto zake linafanyika kwa ushirikiano baina ya Wizara yake na
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Makazi (UN Habitat) na
kuhusisha wadau kutoka mamlaka za upangaji nchini. Kwa mujibu wa
Mahenge, Mjadala huo unaangalia fursa na changamoto zinazopatikana
kutokana na ukuaji Miji na jinsi ya kutumia fursa kuwa na miji endelevu.
Hata hivyo,
Mahenge alisema kwa sasa idadi ya makazi holela imeanza kupungua nchini
kutokana na jitihada za serikali kuruhusu kampuni binafsi za upangaji na
upimaji kushiriki katika kupanga na kupima maeneo mbalimbali ya nchi.
No comments :
Post a Comment