Friday, January 10, 2020

RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN AFUNGUA BARABARA YA KIWANGO CHA LAMI KUTOKA BUBUBU HAHI MKOKOTONI



RAIS wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria kuifungua barabara ya Bububu hadi Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja, iliojengwa kwa kiwango cha lami na Kampuni ya (CCECC ) kutoka Nchini China, ufunguzi huo umefanyika katika eneo la kwa Nyanya (chuini) Wilaya ya Magharibi “A”Unguja ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar.Ndg. Mustafa Aboud Jumbe, akitoa maelezo ya ramani ya barabara baada ya kuifungua leo katika eneo la kwa Nyanya Chuini ,ikiwa ni shanrashamra za kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar.Ndg. Mustafa Aboud Jumbe,(kulia kwa Rais)  akitoa maelezo ya ramani ya barabara baada ya kuifungua leo katika eneo la kwa Nyanya Chuini ,ikiwa ni shanrashamra za kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar.Mhe.Dkt. Sira Ubwa
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akikata uteke kuashiria kuifungua barabara ya Bububu hadi Mkokotoni iliyojengwa kwa kiwango cha lami na kampuni ya Ujenzi kutoka Chini ya  (CCECC) (kulia kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar.Mhe.Dkt, Sira Ubwa na Mwakilishi wa Kampuni ya Ujenzi ya Kanda ya Afrika Mashariki Bw.Zhang Junle na (kushoto kwa Rais) Katibu Mkuu Ndg. Mustafa Aboud Jumbe na Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Meneja Mkaazi Bw.Alex,M.Mubiru.(Picha na Ikulu)

No comments :

Post a Comment