Katibu Mkuu wa wizara ya Madini,
Prof Simon Msanjila wakati akifungua semina ya watendaji wa mamlaka
husika kuhusu uendelezaji,uchimbaji wa madini ya urani na usalama wake
iliyofanyika kwenye jengo la TACAIDS jijini Dar es salaam leo.
Katibu Mkuu wa wizara ya Madini,
Prof Simon Msanjila wakati akifungua semina ya watendaji wa mamlaka
husika kuhusu uendelezaji,uchimbaji wa madini ya urani na usalama wake
iliyofanyika kwenye jengo la TACAIDS jijini Dar es salaam leo kulia ni
Mkurugenzi Prof. Lazaro Busagala Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za
Atomiki (TAEC)

Atomiki (TAEC) na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ,Danny Nyambo
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo.
Baadhi ya watoa mada kutoka jumuiya ya Ulaya wakiwa tayari kwa kutoa mada katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo kutoka wizara na taasisi mbalimbali walioshiriki katika semina hiyo.
Katibu Mkuu wa wizara ya Madini,
Prof Simon Msanjila akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina
hiyo baada ya kuifungua rasmi leo.
…………………………………………………
Katibu Mkuu wa wizara ya Madini,
Prof Simon Msanjila amesema mpaka sasa , wizara ya madini imetoa leseni
moja tu kwa kampuni ya Mantra ili kuchimba madini lakini hata hivyo
uchimbaji wake haujaanza kutokana na kutokamilisha vigezo na masharti ya
sheria.
Prof Simon Msanjila ameyasema
hayo wakati akitoa msimamo wa Serikali kuhusu uchimbaji wa madini ya
Urani kwa ajili ya nishati mbadala wakati akifungua semina ya watendaji
wa mamlaka husika kuhusu uendelezaji,uchimbaji wa madini ya urani na
usalama wake,
Amesema madini hayo yataanza
kuchimbwa baada ya kampuni ya Mantra iliiliyopewa leseni kukamilisha
sheria na taratibu walizotakiwa kuzitekeleza na serikali.
Amesema itafika wakati kampuni
hiyo itakidhi vigezo na wataanza kuchimba na kuendeleza madini hayo
yaliyogundulika kwa wingi katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma hivyo
lazima nchi kuanza kujiandaa na kuandaa wananchi kwa kuwapa
uelewa kuhusu madini hayo.
“Tunajua madini haya
yanaweza kutumika kwa nia nzuri kama kuzalisha nishati na nia nyingine
ikiwemo kutengeneza silaha na mabomu lakini kama nchi bado msimamo wetu
wa kuzalisha nishati kwa njia mbadala hivyo uchimbaji wa madini ya urani
utafuata sheria inayosimamia madini mengine”alisema Profesa Msanjila
Katibu Mkuu amesisitiza kuwa
ufahamu kwa watanzania kuhusu mazingira na usalama unaoendana na
uchimbaji na matumizi ya urani utasaidia kuwa waelewa na ikifika wakati
yakianza kuchimbwa wawe wameishajua yanavyochimbwa na usalama wao.
“Kuna umuhimu wa kuhakikisha
elimu kwa wananchi inafanikiwa kwani madini hayo uchimbaji wake
unatakiwa kufanyika kwa uangalizi wa pamoja huku raia wanatakiwa kuelewa
faida na madhara ya madini kama yasipochimbwa kwa umakini kwa kufuata
taratibu za usalama”amesema
Alisema utakapofika wakati wa
uchimbaji wa madini hayo na kubainika kuna uhitaji wa kutungia sheria
nyingine zitatungwa kwa wakati huo kuangalia manufaa ya nchi na
watanzania.
Naye Mkurugenzi Mwezeshaji wa
Kampuni ya Mantra Tanzania iliyopewa leseni ya kuchimba madini
hayo, Frederick Kibodya alisema licha ya kukamilika kwa baadhi ya
taratibu uchimbaji wa madini hayo utafanyika baada ya bei katika soko la
dunia kufikia kiwango cha kulipa gharama za uendeshaji kwani kwa sasa
bei iko chini ziko chini ambapo wanatarajia bei kuongezeka baada ya
miaka mitatu hadi minne.
Alisema kwa makadirio inaonekana
bei katika soko la dunia itafikia kiwango stahiki baada ya miaka mitatu
hadi minne na kuanza uzalishaji katika eneo hilo la Namtumbo mkoani
Ruvuma.
Alisema baada ya utafiti wa kina kuhusu mradi huo kwa sasa wanachofanya ni kuuendelezwa kwa ajili ya uzalishaji na maandalizi ya msingi tayari yamekamilika ikiwemo kupata vibali ambavyo ni kibali kutoka wizara ya Madini,Kibali cha mazingira kutoka Baraza la taifa la Hifadhi ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC) .

“Bado kibali cha mazingira kutoka
wizara ya maliasili na utalii kutokana na kuwa baadhi ya sehemu
yalipogundulika madini hayo yapo katika hifadhi ya taifa ya selous
iliyopitishwa hivi karibuni “Alibainisha
No comments :
Post a Comment