Thursday, January 30, 2020

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO KUPOKEA ZAIDI YA SH.104.6 MWAKA WA FEDHA 2020-2021



*************************
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, inatarajia kukusanya au kupokea zaidi ya sh. milioni 104.6 katika mwaka wa fedha wa 2020/2021.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Beatrice Dominic wakati akisoma rasimu ya mpango wa Bajeti ya halmashauri hiyo kwa kipindi cha Julai 2020-Juni 2021 kwenye
Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani, uliofanyika leo.
Mkurugenzi huyo amesema, katika fedha hizo ambazo ni Sh. 104,644,876,344.86 Manispaa hiyo itapata Sh. 81,995,999,669.86 ambazo zitakuwa ni ruzuku kutoka Serikali Kuu, Sh. 20,002,948,852 fedha za makusanyo ya ndani Halmashauri hiyo, Sh. 1,895,927,823 kutoka kwa wafadhili na Sh. 750,000,000 zitatokana na michango ya nguvu za wananchi.
Amesema, makadirio ya Bajeti hiyo ya 2020/2021 imeongezeka mwa kiasi cha Sh. 22, 791,778,974.86 ikiwa ni sawa na asilimia 27.8 ikilinganishwa na makadirio ya bajeti inayoendelea ya mwaka 2019/2020.
Mkurugenzi Beatrice amesema katika mchanganuo wa fedha ambazo Halmashauri ya Manispaa hiyo itapata ni kwamba Fedha za ruzuku kutoka Serikali kuu ndizo nyingi zaidi ambapo zitakuwa asilimia 78, wakati Mapato ya ndani ni asilimia 19, za wafadhili asilimia 2 na mchango ya wananchi itakuwa ni asilimia moja tu.
Mkurugenzi huyo amesema, katika mwaka wa fedha wa 2020/2021, Halmashauri ya manispaa ya Ubungo inatarajia kutumia kiasi cha fedha cha sh. 104,644,876,344.86 ambapo kati ya fedha hizo, Sh. 88,599,143,250.86 ni matumizi ya kawaida na mishahara ambayo ni sawa na asilimia ya bajeti yote.
Amesema sh. 16,045,816,960 ni fedha zitakazotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo ni sawa na asilimia 15 ya bajeti yote na kwamba fedha hizo zitakazotumika katika miradi ya maendeleo zinajumuisha kiasi cha sh. 8, 516,769,314.
Mkurugenzi huyo amesema bajeti hiyo imelenga katika kuboresha maisha ya wananchi na kukuza kipato cha mkazi ili kukuza uchumi wa ndani na kwamba miongoni mwa vipaumbele vya Halmashauri ya Manispaa hiyo itakuwa ni kuimarisha utawala bora, na uhtoaji huduma kwa jamii kwa kujenga ofisi tisa za mitaa, ujenzi wa Jengo la halmashauri na ununuzi wa gari la Idara ya Utawala.
Amesema kwa upande wa Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge na madiwani, Halmashauri hiyo ya Manispaa ya Ubungo itatumia sh. milioni 240, kusimamia uchaguzi huo

No comments :

Post a Comment