Naibu Katibu Mkuu Afya Ofisi ya
Rais TAMISEMI, Dkt. Dorothy Gwajima akiwa anakagua jengo jipya la
upasuaji la Kituo cha Afya mkoani ambapo ametoa siku 14 kiwe kimeanza
kazi. (Picha na OR-TAMISEMI)
Muonekano wa jengo jipya la upasuaji kituo cha Afya mkoani katika Halmashsuri ya Mji Kibaha, Pwani.
**************************
Na. Atley Kuni Kibaha- PWANI
Mganga Mfawidhi
wa Kituo cha Afya Mkoani kilichopo mkoani Pwani katika Halmashuri ya
Kibaha Mji Dkt. Godfrey Kajungu, amesema kuwa wamejizatiti kuongeza wigo
wa utoaji wa
huduma za upasuaji katika kituo hicho mara baada ya
serikali kuwapatia Milioni 500 katika awamu tatu ya mpango wa serikali
wa kuimarisha miundombinu ya Afya nchini.
Akizungumza muda
mfupi mara baada ya Ziara ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI,
anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy Gwajima, Daktari Kajungu alisema
kituo ca Afya cha mkoani ni moja vituo tegemeo katika Wilaya hiyo
kutokana na kuhudumia wananchi zaidi 100 kwa siku wanaofika kwa matatizo
mbalimbali ya kiafya.
“Kama mlivyosikia
Naibu Katibu Mkuu ameagiza ndani ya wiki mbili jengo hili la upasuaji
liwe limeanza kazi, sisi tunamthibitishia kuwa ifikapo tarehe 09
Februari, 2020 tutaanza shughuli za upasuaji katika jengo hili jipya ili
kuwarahisishia wananchi huduma za afya.” Alisema Dkt. Kajungu.
Akizungumza mara
baada ya kutembela majengo hayo mapya yaliyopokea milioni 500 mwezi
Mei,2028 kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa baadhi ya huduma, Naibu
Katibu Mkuu Dkt. Dorothy Gwajima, aliutaka uongozi wa kituo hicho kuanza
kutoa huduma hasa ikizingatiwa kuwa kituo hicho kipo umbali wa mita
zisizozidi mita 400 hivyo uwepo wa huduma za upasuaji ni muhimu katika
kuokoa maisha endapo dharura imetokea, lakini pia kituo hicho kwa sasa
ndio kinatumika kama Hospitali ya Wilaya hadi hapo Hospitali ya Wilaya
itakapo kamilika.
Kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa na Mganga mfawidhi wa kituo hicho, kituo cha Afya
mkoani kina jumla ya Madaktari 9, madaktrari wasaidizi 4, Matabibu 4 na
Maafisa wauguzi 3 Wauguzi wasaidizi 20, Wakunga 19 wataalamu wa maabara
10 na wataalamu wa Utrasound 2 idadi ambayo imetajwa kukidhi mahitaji
kwa sasa.
Naibu katibu mkuu
yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi kukagua huduma za Afya, ikiwa ni
muendelezo wa kuhakikisha katika kila kituo na Hospitali huduma za Afya
zinatolewa kwa ubora ili wananchi waendelee kuvutiwa na kuendelea
kuziamini Hospitali na Vituo hivyo kwani hali ya upatikanaji wa huduma
kwa sasa imezidi kuboreshwa katika awamu hii ya tano.
No comments :
Post a Comment