Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally, amepokea
mapendekezo ya Ilani ya mwaka 2020 – 2025 kutoka kwa Jumuiya ya Walemavu
Nchini.
Mapendekezo hayo yametolewa kwa wajumbe na wananchi wote wenye ulemavu kutoka kanda tisa nchini
Makabidhiano hayo yamefanyika jioni ya leo tarehe 30 Januari, 2020 Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma.
Katika makabidhiano hayo, wajumbe
wa Jumuiya hiyo wameishukuru na kuipongeza CCM na Serikali yake,
inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, kwa kuwajali na kuweka sera
rafiki na wezeshi kiuchumi, kijamii na siasa ikiwa ni pamoja na
kuwazingatia katika nafasi mbalimbali za uongozi.
Jumuiya hiyo imeongozwa na Mwenyekiti Ndg. Peter Sarungi akiwa na viongozi na wajumbe mbalimbali.
Huu ni muendelezo wa CCM kupitia
Ofisi ya Katibu Mkuu kupokea mapendekezo mbalimbali kuelekea kuandika
Ilani mpya Jumuishi ya Uchaguzi Mkuu kwa Mwaka 2020 – 2025, kutoka
kwenye Taasisi, mashirika, vyama vya siasa na vya kijamii nchini,
makundi ya wasomi na watu binafsi.
No comments :
Post a Comment