Friday, January 10, 2020

OPARESHENI YA KUPAMBAMBANA NA VIKUNDI VYA KIHARIFU



Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Morogoro (SACP)  Wilbroad Mtafungwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Watuhumiwa wanajihusisha na vikundi vya uharifu, wanaojiita  samaki poli na damu chafu wakiwa kituo cha Polisi Mkoa wa Morogoro 
……………………………
Na farida saidy,Mororgoro 
Kutokana Na Matukio Mbalimbali Ya Uharifu Yaliojitokeza Hivi Karibuni Katika Kata Ya
Tubuyu Manispaa Ya Morogoro Na  Vikundi Vinavyojita Samaki Poli Na Damu Chafu, Jeshi La Polisi Mkoani Morogoro Limeanzisha Opareshini Kabambe Ya kutokomeza Vikundi Vyote Vinavyojihusisha Na Shuhguri Hizo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini Kwake Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Morogoro (SACP)  Wilbroad Mtafungwa Amesema Vikundi Hivyo Vinajihusisha Na Uporaji ,Utumiaji na Uuzaji Wa Bhangi,AMBAPO wamekutwa na misokoto 173 bhangi.
Aidha kamanda amesema jeshi la polisi linawashirikili watu 8 ambao wanajihusisha na vikundi hivyo,na katika mahujiano wamekiri kufanya shughuri hizo,ambapo hatua za kuwapeleka mahakamani zinafuata.
Hata Hivyo Amewataja Watu Hao Kuwa Ni Saidy Omary 31mussa Mohamedi 28 Abdallah Adamu 39 Issa  Saidy 32 Bakari Athumani 28 Amani Zebeda 33 Na Omary Kessy 25,sambamba na kuwataka viongozi wa serikali za mtaa kusimamia swala zima la ulinzi na usala wa mtaa husika.

No comments :

Post a Comment