Friday, January 10, 2020

WAZIRI UMMY ATOA MILIONI 2.5 KWA AJILI YA USHONAJI WA SARE 100 ZA WATOTO YATIMA SHULE YA MSINGI JIJINI TANGA

 MBUNGE
wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akimkabidhi fedha
Taslimu kiasi cha Milioni 2.5 Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushonaji cha
Vijana cha Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai) Liliani Michael kwa
ajili ya kushona sare 100 za watoto yatima wa shule za Msingi Jijini
Tanga ambapo fedha hizo zimetolewa na Mbunge Ummy
 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto
akisisitiza jambo mara baada ya kukabidhi fedha Taslimu kiasi cha Milioni 2.5 Mwenyekiti wa Kikundi
cha Ushonaji cha Vijana cha Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai)
Liliani Michael kwa ajili ya kushona sare 100 za watoto yatima wa shule
za Msingi Jijini Tanga ambapo fedha hizo zimetolewa na Mbunge Ummy
 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto
akisisitiza jambo mara baada ya kukabidhi fedha Taslimu kiasi cha Milioni 2.5 Mwenyekiti wa Kikundi
cha Ushonaji cha Vijana cha Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai)
Liliani Michael kwa ajili ya kushona sare 100 za watoto yatima wa shule
za Msingi Jijini Tanga
ambapo fedha hizo zimetolewa na Mbunge Ummy

 MBUNGE
wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto
akizungumza jambo mara baada ya kukabidhi fedha Taslimu kiasi cha
Milioni 2.5 Mwenyekiti wa Kikundi
cha Ushonaji cha Vijana cha Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai)
Liliani Michael aliyesimama kulia kwa ajili ya kushona sare 100 za
watoto yatima wa shule
za Msingi Jijini Tanga
ambapo fedha hizo zimetolewa na Mbunge Ummy
 MBUNGE
wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto
akiangalia nguo ambazo zinashonwa na kikundi hicho mara baada ya
kukitembelea kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi hicho Lilian Michael
 MBUNGE
wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akiteta
jambo Mwenyekiti wa Kikundi
cha Ushonaji cha Vijana cha Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai)
Liliani Michael mara baada ya kukabidhi fedha Taslimu kiasi cha Milioni
2.5 Mwenyekiti kwa ajili ya kushona sare 100 za watoto yatima wa shule
za Msingi Jijini Tanga kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias
Mwilapwa na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
 MBUNGE
wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akitazama
nguo ambazo zinashonwa na  Kikundi
cha Ushonaji cha Vijana cha Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai)
mara baada ya kukabidhi fedha Taslimu kiasi cha Milioni 2.5 Mwenyekiti
wa Kikundi hicho Lilian Michael kwa ajili ya kushona sare 100 za watoto
yatima wa shule
za Msingi Jijini Tanga kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias
Mwilapwa na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
 MBUNGE
wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto
akiangalia nguo zinazoshonwa na kikundi Ushonaji hicho mara baada ya
kukitembela kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na
katikati mwenye shati jeuzi na mistari ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga
Daudi Mayeji
 MBUNGE
wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akiteta
jambo na Mwenyekiti wa Kikundi
cha Ushonaji cha Vijana cha Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai)
Liliani Michael mara baada ya kukabidhi fedha Taslimu kiasi cha Milioni
2.5 Mwenyekiti kwa ajili ya kushona sare 100 za watoto yatima wa shule
za Msingi Jijini Tanga kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias
Mwilapwa na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
MBUNGE
wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya MAendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto ametoa sh.milioni 2.5 kwenye kikundi cha ushonaji cha Vijana
Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai) kwa ajili ya kushona sare 100 za
wanafunzi yatima wa shule za Msingi Jijini Tanga.
Fedha
hizo zimekabidhiwa na Waziri Ummy kwa Mwenyekiti wa Kikundi hicho Lilian
Michael wakati alipotembelea na kujionea namna wanavyofanya shughuli zao
ikiwemo changamoto ambazo wanakabiliana nazo huku akihaidi kushirikiana nao.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi fedha hizo, Mbunge Ummy alisema ametoa fedha ili kuweza
kuwasaidia wanafunzi hao ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana
na kukosa wazazi ambao wanaweza kuwanunulia.
“Niwapongeze
kwa kazi nzuri mnayoifanya hapa kwenye kikundi chenu mimi nitawaunga mkono na
leo nitawakabidhi milioni 2.5 kwa ajili kuwashonea sare watoto yatima 100
kwenye Jiji la Tanga”Alisema Waziri huyo
.
Aidha
pia alimtaka Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji waweke utaratibu wa watoto
wanaoanza darasa la kwanza shule za msingi wapate unifomu shuleni kwa kushonewa
na kikundi hiki cha vijana cha Tanga Youth Tailoring Industry (Tayotai).
“Kutokana
na kwamba kikundi hiki kinafanya kazi nzuri hivyo wapeni tenda ya ajira kwani
mtaji umewekwa na vifaa vipo suala lingine ni kutoa maelekezo watoto wanaonza
darasa la kwanza kupata sare shuleni “Alisema
Waziri
huyo alisema kwamba kikundi hicho walipewa mkopo wa milioni 100 huku akieleza
kwamba sera ya maendeleo ya wanawake ambao ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato
ya ndani ya Halamshauri ipo chini ya wizara yake.
Alisema
kwamba wasije kuwaambia Halmashauri watoe mikopo lakini hatuoni maendeleo kwenye
hili huku akiwapongeza Jiji hilo kwa kutekeleza sheria ya kutenge fedha kwa
ajili ya wakina mama vijana na watu wenye walemavu.
Waziri
huyo alisema kwamba fedha hizo zimetoka kwa kununua vifaa na ela za uendeshaji huku
akimtaka Mwenyekiti wa Kikundi hicho kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi
mkubwa ili matokeo yake yaanze kuonekana.
“Kwa
sasa hiyo milioni 100 mliopata kutoka Halmashauri tunachotaka irudi waweze kukopeshwa
kikundi kingine sasa tumepeana muda kwa mwenendo walionao nawaombea waongezewe
muda ili waweze kurejesha fedha hizo “Alisema Waziri Ummy
Awali akizungumza
wakati akitoa taarifa ya mradi wa ushonaji wa Kikundi cha Vijana cha Tanga
Youth Tailoring Industry (Tayotai) Mwenyekiti wa Kikundi hicho Liliani Michael
alimshukuru Waziri Ummy kwa kuwasaidia kwenye kikundi hicho ambalo alisema
kimeanzishwa mwezi Machi 2019 kikiwa na jumla ya wanachama 32 wakiwa ni
wasichana.
Alisema
kikundi hicho kinajishughulisha na ushonaji wa cherehani ambapo kinashona nguo
na mitindo tofauti kwa makundi yote huku akieleza lengo la mradi huo ni
kuimarisha maisha ya wanachama kiuchumi na kijamii.
“Lakini
pia kutoa suluhisho la tatizo la ajira kwa vijana ikiwemo kusaidia kutatua
changamoto za kijamii sambamba na kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya serikali
ya awamu ya tano inayo ongozwa na Rais Dkt John Magufuli kuelekea uchumi wa
viwanda kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025”Alisema
Mwenyekiti
huyo alisema kwamba ili kufikia malengo yao waliwa silisha maombi kwa
Halamshauri ya Jiji la Tanga ili wapatiwe mkopo kupitia asilimia 10 ya mapato
yake ya ndani.
“Hivyo
Halmashauri imetupatia mkopo wa milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya
ushonaji vya kisasa pamoja na mtaji wa kuanzia biashara kupitia mkopo
Halmashauri ilikiwezesha kikundi chetu kwa kutununulia vifaa kama vile
Cherahani za kisasa za kushonea 35, Overlock 1, Mashine ya kudarizi mashuka na
vitambaa 3, kudarizi nguo 2, kufuma masweta 2,kuweka nembo 2,kushona vifungo
1,kugongesha vifungo 3 na kutupatia fedha taslimu kwa ajili ya uendeshaji “Alisema

No comments :

Post a Comment