Akipanda mti kuashiria uzinduzi
kulia kwake ni mmiliki wa shamba Bi Desderia Komba ambaye amehamasika
kulima zao hilo kutokana na maboresho ya serilali ya awamu ya tano..
Ofisa kilimo wa kata ya
Kingerikiti Wilayani hapa Richard Katale (Mwenye kanzu) ambaye pia ni
mkaguzi wa zao la kahawa wilayani Nyasa, akitoa mafunzo kwa wakulima wa
zao la kahawa juu ya upandaji miche mipya, ya kahawa aina ya Compact
kabla ya kuwagawia wakulima waweze kupanda miche hiyo hivi karibuni
katika Kata ya Kingerikiti Wilayani Nyasa.

Mkuu wa Idara ya Kilimo,
Umwagiliaji na ushirika Menance Ndomba, (mwenye shati jeupe)
aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela chilumba, akigawa
miche ya kahawa katika uzinduzi wa ugawaji miche mipya ya Kahawa, aina
ya Compact kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa, uzinduzi uliofanyika hivi
karibuni katika kijiji cha Kingerikiti na Kata ya Kingerikiti Wilayani
Nyasa.
…………………………………………………………………………………………………
Wakulima wa zao la kahawa Wilayani
Nyasa, kwa kushirikiana na Vyama vya Msingi vya
mazao na watu binafsi,
wamezalisha miche ya kahawa 262,500 kwa msimu wa kilimo 2019/2020 ili
kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa na kukuza uchumi wa wananchi.
hayo yamesemwa na wakulima wa zao
la kahawa katika Risala yao, kwa mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi
Isabela O.Chilumba, wakati akizindua ugawaji wa miche mipya ya kahawa
aina ya “Compact” Uzinduzi uliofanyika Hivi karibuni, katika Kijiji cha
Kingerikiti Kata ya Kingerikiti Wilayani hapa.
Wakulima hao wamefafanua kuwa,
wamelazimika kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa ikiwa ni pamoja, na
utekelezaji wa Agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh.Cassim Majaliwa aliyezitaka kili Halmashauri Nchini kuzalisha miche
ya kahawa zaidi ya laki mbili.
Waliongeza kuwa Vyama saba vya
Ushirika wa mazao vimezalisha miche hiyo na tayari kwa kugawa kwa
wananchi kwa mchanganganuo ufuatao Nambawala AMCOS (10250), Kingerikiti
AMCOS miche( 37,705), Tingi AMCOS (4,300) LIPO AMCOS MICHE (40,000),
Mapendo AMCOS Miche (36,000) na Luhangarasi AMCOS 9890.
Pia wakulima hao walikipongeza
kituo cha utafiti cha Ugano (TACRI) kwa kuwagawia bure miche kahawa
18,200 aina ya compact, ambayo wameigawa kwa wakulima ambao wanauhitaji
wa miche hiyo.
Akitoa maelekezo ya upandaji wa
miche hiyo kwa wakulima wa zao la kahawa, Ofisa kilimo wa Kata ya
Kingerikiti ambaye pia ni Mkaguzi wa zao la Kahawa Bw.Richard Katale,
aliwataka wakulima, kulihudumia vizuri, kwa kupanda kwa nafasi ya Meta
mbili na kwa Hekari moja watapanda meche mia sita.
Aliongeza kuwa sifa za mche wa
compact unazaa mapema na unavumilia ukame. Alikawataka wananchi kupanda
kwa maelekezo aliyoyatoa, ili kufikia uzalishaji wenye tija kwa kuwa
Serikali imedhamiria kuboresha maisha ya wakulima wa zao la Kahawa.
Aidha wakulima hao, waliipongeza
Serikali ya awamu ya tano kwa kufanya maboresho mbalimbali ya zao la
kahawa, na kuwaletea mnada wa kahawa katika Wilaya ya Mbinga na
kuwapunguzia usumbufu kwa kuwa awali walikuwa wakienda moshi kufanyia
mnada.
“kwa kweli awamu hii tunaona jinsi
gani Serikali inatujali wakulima, kwa kuwa tunapewa mafunzo ya kulima
kahawa, lakini pia kitendo cha kutupa miche ya ya kahawa bure , Serikali
imetusaidia sana. Nimejaribu kupanda na nimeona ni mbegu nzuri inayotoa
mavuno mengi kwa muda mfupi ukilinganisha na kahawa tuliyozoea kupanda
awali”. Alisema Bonus mapunda mkulima wa zao la kahawa kutoka katika
kijijii cha kingerikiti.
Akizungumza na wakulima wa zao la
Kahawa Wilayani hapa, Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
Bw.Menance Ndomba aliyemwakilisha mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi,Isabela
Chilumba,Aliwapongeza wakulima wa Zao la kahawa Wilayani Nyasa, kwa
juhudi wanazozifanya za kulima na kutunza zao hilo na kuinua mapato ya
Halmashauri na kuwa na kipato bora cha Familia na kuchangia maendeleo
mbalimbali katika maeneo yao.
Aidha aliwataka kuendelea kuongeza
uzalishaji wa zao la Kahawa kwa kuwa , Wilaya ya Nyasa ina Fursa ya
mashamba makubwa, kwa mujibu wa Utafiti uliofanyika hivi karibuni na
“CAFE Afrika” katika Wilaya ya Mbinga na Nyasa Wilaya ya Nyasa ina fursa
kubwa ya kupanua mashamba ya kahawa ukilinganisha na Wilaya ya Mbinga.
“nachukua fursa hii kuwapongeza
sana wakulima wa zao la kahawa Wilayani Nyasa, kwa kazi nzuri
mnayoifanya ya kujituma kulima na kuzalisha zao hili la kahawa ambalo
linatupa faida kubwa sana katika Halmashauri yetu kama vile ,mapato ya
ndani na mnachangia maendeleo mbalimbali katika maeneo yenu.Serikali ipo
pamoja nanyi na itatatua changamoto mbalimbali mtakazokutana nazo
katika shughuli zenu na kuhakikisha Miundombinu inajengwa. Alisema
ndomba.
Wilaya ya Nyasa ipo katika Mkakati
wa kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara ya Kahawa,kakao, na korosho
ili kukuza uchumi wa kipato cha mwananchi mmoja mmoja na Wilaya kwa
ujumla.
No comments :
Post a Comment