Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya
Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akisisitiza umuhimu
wa Mipango ya kujiandaa na kukabiliana na maafa ya Mikoa linakopita
Bomba la Mafuta, kuzingatia athari zinazoweza kujitokeza na kuathiri
Mradi huo, wakati alipotembelea eneo la kwenye peninsula ya Chongoleani
karibu na bandari ya Tanga ambapo utekelezaji wa Mradi huo utatekelezwa
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya
Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akisisitiza umuhimu
wa Mipango ya kujiandaa na kukabiliana na maafa ya Mikoa linakopita
Bomba la Mafuta, kuzingatia athari zinazoweza kujitokeza na kuathiri
Mradi huo, wakati alipotembelea eneo la kwenye peninsula ya Chongoleani
karibu na bandari ya Tanga ambapo utekelezaji wa Mradi huo
utatekelezwa..
Kaimu Katibu Tawala, Mkoa wa
Tanga, Noel Kazimoto, akimueleza Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya
Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe umuhimu wa Mpango wa
kujiandaa na kukabiliana na maafa wa Mkoa huo linakopita kuzingatia
athari zinazoweza kujitokeza na kuathiri Bomba la Mafuta , wakati
walipotembelea eneo la kwenye peninsula ya Chongoleani karibu na bandari
ya Tanga ambapo utekelezaji wa Mradi huo utatekelezwa.
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya
Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe na Kaimu Katibu
Tawala, Mkoa wa Tanga, Noel Kazimoto, wakisoma Jiwe la uzinduzi wa
utekelezaji wa Mradi wa Bomba la mafuta, wakati walipotembelea eneo la
kwenye peninsula ya Chongoleani karibu na bandari ya Tanga ambapo
utekelezaji wa Mradi huo utatekelezwa na kushauri mipango ya menejimenti
ya maafa ya mikoa linakopita bomba hilo izingatia athari zinazoweza
kujitokeza na kuathiri mradi huo.

Mkurugenzi
Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy
Matamwe akiangalia sehemu ya peninsula ya Chongoleani karibu na bandari
ya Tanga wakati alipotembelea eneo la utekelezaji wa Mradi wa Bomba la
Mafuta, ambapo ameshauri mikoa linakopita Bomba hilo kuzingatia
Mradi huo katika mipango ya menejimenti ya maafa kwa athari zinazoweza
kujitokeza na kuathiri mradi huo.
…………………………………………………………………………………….
Ofisi ya Waziri
Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, imezishauri Kamati za Usimamizi wa
Maafa katika mikoa 8 na vijiji 184 vinavyopatikana katika wilaya 24
zilizopo katika mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida,
Dodoma, Manyara na Tanga, ambapo Mradi wa Bomba la Mafuta utatekelezwa
kuuweka Mradi huo katika Mipango yao ya kujiandaa na kukabiliana na
Maafa ili kuhakikisha mradi huo hauthiriwi na majanga yanayoweza
kutokea.
Kwa mujibu wa
sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015, inaainisha majukumu
ya kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi mkoa,
ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, jukumu la msingi ni kutoa taarifa za
tahadhari ndani ya eneo husika, Kuratibu na kusimamia shughuli za
usimamizi wa maafa na operesheni za dharura ndani ya Kijiji wilaya au
mkoa, pamoja na kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa
katika ngazi husika.
Akiongea mara
baada ya kutembelea eneo la kwenye peninsula ya Chongoleani karibu na
bandari ya Tanga ambapo utekelezaji wa Mradi huo utatekelezwa,
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali
Jimmy Matamwe amefafanua kuwa Kamati za maafa zinalo jukumu la kuchukua
tahadhari ya namna ya kuhakikisha majanga yanayoweza kuuathiri mradi huo
yanakuwa katika mipango yao ya menejimenti ya maafa ili faida
zitakazotokana na utelelezaji wa mradi huo zinakuwa endelevu.
Kwa upande
wake, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Noel Kazimoto ameeleza kuwa
utekelezaji wa mradi huo utafungua fursa za kiuchumi kwa watanzania
hivyo ni dhahiri kuwa eneo la Chongoleani litakuwa na mwingiliano mkubwa
wa watu na shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii zitakuwa
zikiendeshwa, kwa kuwa wananchi ni wadau wa menejimeti ya maafa kupitia
kamati za menejimenti za maafa kuanzia ngazi ya vijiji, wataendelea
kuelimishwa juu ya majanga yanayoweza kuuathiri mradi huo ili waweze
kuhakikisha mradi unakuwa endelevu.
Kwa mujibu wa Tovuti rasmi ya Kampuni inayojenga mradi huo, East African Crude Oil Pipeline www.eacop.com.
Kampuni hiyo inabainisha kuwa wanao mpango unaohakikisha utelezaji wa
mradi huo unazingatia majanga na maafa wakati wa kupanga, kujenga na
kuendesha Bomba, ambapo Mpango huo unahakikisha kwamba, katika tukio la
dharura linaloweza kutokea, hatua za haraka, zinachukuliwa.
Mradi wa
Bomba la Mafuta Ghafi unatekelezwa kwa ubia wa ujenzi na uendeshaji kwa
kushirikisha kampuni za Total ya Ufaransa, CNOOC ya China, Tullow ya
Uingereza na Serikali za Tanzania na Uganda. Mafuta ghafi yatasafirshwa
kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi bandari ya
Tanga nchini Tanzania. Mradi wa Bomba hilo una umbali wa kilometa 1,445
ambapo kilometa 298 zitakuwa nchini Uganda, na kilometa 1,147 zitakuwa
nchini Tanzania
No comments :
Post a Comment