Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akikaribishwa rasmi
katika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dodoma. Wengine katika picha ni
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo na Balozi
Joseph Sokoine Naibu Katibu Mkuu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongea na
Menejimenti ya Ofisi yake mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo
katika Mji wa Serikali Mtumba mapema leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongea na sehemu
ya watumishi wa Ofisi yake mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo
katika Mji wa Serikali Mtumba mapema leo. Pamoja na mambo mengine
amewasisitiza watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia
Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo.
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais ambae sasa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.
George Simbachawene akimkabidhi rasmi Ofisi Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu.
Makabidhiano hayo yamefanyika hii leo katika Mji wa Serikali Mtumba –
Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Mhe. George Simbachawene mara baada ya kukabidhiana Ofisi hii leo Mtumba
Dodoma. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais
Mhandisi Joseph Malongo, Naibu Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine na
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
nchini (NEMC) Dkt. Samwel Mafwenga
…………………………………………………………………………….
Na Lulu Mussa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu amemtaka kila
mtumishi katika Ofisi ya Makamu wa Rais atimize wajibu wake katika
kuleta maendeleo ya Taifa letu.
Hayo ameyasema hii leo mara baada
ya kuwasili rasmi katika Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali
Mtumba Dodoma na kupokewa na Menejimenti na watumishi na Ofisi hiyo.
Akizungumza na watumishi wa Ofisi
yake Waziri Zungu amewataka wote kufanya kazi kwa ushirikiano na kuahidi
kuendelea kusimamia Sheria, Taratibu na Kanuni zilizopo.
Ametoa rai kwa watanzania kuwa
chachu ya mabadiliko katika kuhifadhi na kusimamia Mazingira. “Simamieni
Sheria bila kumuonea mtu, pale ambapo Sheria imekataza jambo simamieni
Sheria na kuchukua hatua kwa wote wanaokiuka” Zungu alisisitiza.
Awali aliyekuwa Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ambae sasa ni wa Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene amekabidhi Ofisi
rasmi kwa Waziri Zungu na kumtakia kila la heri katika kutekeleza
majukumu yake mapya.
“Tumefanikiwa katika katazo la
mifuko ya plastiki, tumeridhia Mikataba na Itifaki mbalimbali na pia
tuna program maalumu ya Upandaji mti nchi nzima ambayo ni endelevu”
Simbachawene alisisitiza.
Pia Mhe. Waziri Simbachawene
alisema kuwa mbali ya kufanikiwa katika kampeni ya katazo la mifuko ya
plastiki lakini zaidi na elimu inapaswa kutolewa kwa wananchi kuhusu
tofauti ya vifungushio na vibebeo ambavyo bado wananchi wanachanganya.
Amempongeza na kumshukuru Katibu
Mkuu wa Ofisi hiyo Mhandisi Joseph Malongo kwa muda aliofanya nae kazi
kwa ukaribu ambapo wameweza kutekeleza majukumu mbalimbali yakiwemo
kuridhia mikataba, itifaki na kanuni zinazohusu mazingira.
Waziri Zungu ameteuliwa hivi
karibuni na Rais Dkt. John Magufuli kushika nafasi hiyo baada ya kufanya
mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri ambapo Mhe. Simbachawene
aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments :
Post a Comment