Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi kuhusu kuacha
tabia ya kuingiza mifugo Hifadhini badala yake waheshimu sheria za
Uhifadhi ambapo alitumia nafasi hiyo kuiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyamapori Tanzania ( TAWA) iachie mifugo zikiwemo ng’ombe 179
zilizokuwa zimekatwa ndani ya Pori la Akiba la Mkungunero katika mkutano
wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kimotorok wilayani Simanjiro
mkoani Manyara
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja
na baadhi ya Wazee maarufu wa Kijiji cha Kimotorok mara baada ya
kufanya mkutano katika kijiji hicho kwa kuiagiza TAWA iachie mifugo
zikiwemo ng’ombe 179 kwa makubaliano ya kutoingiza tena mifugo hiyo
katika Pori la Akiba la Mkungunero.
Mbunge wa Simanjiro akizungumza na
Wananchi kuhusiana na tabia iliyozuka ya kuwavamia na kuwadhuru
Wahifadhi wakati wanapotekeleza majukumu yao na kuwa yeyote
atayethubutu kutenda vitendo hivyo yeye hatakuwa upande wake wakati
akizungumza nao katika mkutano uliofanyika katika kijiji cha Kimotorok
wilayanii Simanjiro katika mkoa wa Manyara.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha
Kimotorok wakimsiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii wakati wa
mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kimotorok ambapo aliwataka
wananchi hao wasiingize mifugo Hifadhini na atakayeingiza mifugo ndani
ya Hifadhi atafrisiwa mifugo yote
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe, Constantine kanyasu akiwa na Wazee maarufu wa Kijiji hicho
mara baada ya kumaliza kwa mkutano ambapo aliruhusu mifugo iliyokuwa
imekamatwa katika Pori la Akiba la Mkungunero iachiwe.
Naibu Waziri wa Maliasili na
utalii mhe. Constantine Kanyasu akiteta jambao na Naibu Kkamishna
Uhifadhi wa TAWA,Mabula Misungwi ( kushoto) wakati wa mkutano wa mkutano
wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kimotorok wilayani Simanjiro
mkoani Manyara, Katika ni Mkurugenzi Mtendaji wa wialya ya Simanjiro,
Yefred Myenzi.
(Picha zote na Wizara ya Maliasili na Utalii)
***************************
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe.Constantine Kanyasu ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori
Tanzania ( TAWA) kuiachia na kuirudisha mifugo zikiwemo jumla ya ng’ombe
179 zilizokuwa zimekamatwa ndani ya Pori la Akiba la Mkungunero ambayo
ni Mali ya Mathayo Marao, Mwananchi wa Kijiji cha Kimotorok kilichopo
ndani ya Pori hilo katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara kwa
makubaliano ya kutoingiza tena mifugo hiyo.
Uamuzi huo umekuja kufuatia utata uliopo eneo
ilipokamatiwa mifugo hiyo kwa vile Kijiji hicho cha Kimotorok ni
miongoni mwa Vijiji na Vitongoji 366 vilivyo ndani Hifadhi na
vinavyosubilia maamuzi ya Rais wa Tanzania, Mhe.John PombeMagufuli na
moja kati ya maagizo aliyoyatoa kwamba wananchi wa Vijiji hivyo
wasibugudhiwe hadi pale maamuzi ya mwisho yatakapotolewa.
Kwa mujibu wa Wahifadhi, Mifugo hiyo
iliyokamatwa mwishoni mwa mwaka jana inadaiwa kukutwa mita 450 ndani ya
Pori hilo huku Wananchi wakidai kuwa Mifugo hiyo ilikutwa nje ya mita
450 kutoka kwenye mpaka mahali ambako wamekuwa wakiishi huku wakisubiri
kauli ya mwisho ya Mhe.Rais.
Mvutano huo baina ya Wahifadhi na Wananchi
umempekelea Mhe.Kanyasu kutumia busara na kufikia uamuzi huo kwa
kuzingatia kuwa Kijiji hicho kipo ndani ya Hifadhi.
Kutokana na majadiliano ya pande hizo mbili,
Naibu Waziri huyo amelazimika kutoa uamuzi huo wa kuachia mifugo hiyo
kwa makubaliano ya Wananchi wa Kijiji hicho kuheshimu sheria za
Uhifadhi kwa kutoingiza mifugo ndani ya Hifadhi hadi pale maamuzi ya
mwisho yatakapotolewa na Rais Magufuli.
Akizungumza jana katika mkutano huo uliofanyika
kwenye Kijiji cha Kimotorok, Naibu Waziri Mhe.Kanyasu amesema uamuzi huo
umefanyika kwa busara kwa vile mifugo hiyo ilibidi ipelekwe mahakamani.
Amesema kitendo cha kuacha kupeleka kesi hiyo
mahakamani kinasaidia kupunguza idadi kubwa ya mifugo kufa ambapo hadi
sasa zaidi ya ndama kumi wameshakufa.
Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu amewataka
wananchi hao kuacha kutumia vibaya kauli ya Rais Magufuli kwa kuanza
kuvamia maeneo mapya ya Hifadhi kwa kisingizio cha kauli hiyo ilhali
wanatakiwa kubaki na mifugo yao mahali walipo.
Amefafanua kuwa kulikuwa na uwezekano wa
kupeleka mifugo hiyo mahakamani ila kutokana na Wananchi hao kuomba
maridhiano kwa kutambua kuwa wametenda kosa imepelekea mifugo hiyo
kuachia.
Katika hatua nyingine, Mhe Kanyasu amesema
Serikali haipendi kutaifisha mifugo inayokamatwa Hifadhini kama sheria
inavyoelekeza kwa vile wananchi wengi wamejikuta kwenye umaskini wa hali
ya juu, Hivyo amewataka wananchi hao kuacha tabia ya kuingiza mifugo
hifadhini kwa vile watafrisiwa.
” Serikali inafurahi kuona Wafugaji wananeemeka
kupitia mifugo yao huku uhifadhi ukiendelea kwa maslahi mapana ya Taifa”
alisisitiza Kanyasu
Aidha, Mhe.Kanyasu ametoa onyo kwa Wananchi
wanaovamia Wahifadhi wakiwa wanatekeleza majukumu yao na kuahidi kuwa
Serikali haitamvumilia Mwananchi yeyote atakayethubutu kutumia mabavu
dhidi ya Wahifadhi.
” Tukikubaini ni miongoni mwa Mwanakijiji
uliyejitokeza ukiwa umeshika mkuki au unapiga mwano kwa nia ya
kuwahamasisha wenzako kwa ajili ya kuwadhuru Wahifadhi,
Tutakushughulikia ipasavyo” Alisisitiza
Kwa upande wake Mbunge wa Simanjiro, Mhe. James Millya amewataka wananchi waache tabia ya kuingiza mifugo ndani ya Hifadhi.
Pia amelaani vikali vitendo vya baadhi ya
wananchi wanaohamasisha ghasia kwa Wahifadhi na kuahidi kuwa yeye
hatakuwa tayari kumsaidia mwananchi yeyote atakayekamatwa kwa kutenda
kosa hilo kwa vile Wahifadhi hao wanafanya kazi za kulinda Hifadhi hizo
kwa niaba ya Watanzania wote.
Kufuatia hali hiyo, Mhe.Millya amewataka Wazee
wa mila ‘Olaibon’ kutumia nafasi hiyo kwa kuitaka jamii yao kufuata
sheria za Uhifadhi kwa kuheshimu Sheria zilizopo zinazokataza kulisha
mifugo ndani ya Hifadhi
Akizungumza kwenye mkutano huo, Mhe.Millya
amewataka Wananchi hao kila mmoja awe Mlinzi wa mwenzake kwa kuimarisha
ujirani mwema kati ya Wananchi na Wahifadhi badala ya kuendekeza uhasama
kwa kuingiza mifugo ndani ya Hifadhi.
Awali, Joseph Olematwaa ambaye ni mkazi wa
Kijiji hicho alisema uamuzi wa kuachia mifugo utarudisha mahusiano mema
kati ya Wahifadhi wa Pori hilo na Wananchi na kuahidi kuwa hawataingiza
tena mifugo ndani ya Hifadhi.
No comments :
Post a Comment