
*****************************
NA ANDREW CHALE, BUSEGA
MJI wa Lamadi uliopo
katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu unatazamiwa kuwa
miongoni mwa miji mikubwa Barani Afrika utakaokuwa ukiingiza fedha
nyingi za kigeni sambamba na kupokea watalii wengi zaidi kwa mwaka,
kutokana na kituo cha michezo cha Maajabu ya Utalii ‘Disneyland’.
Hayo yamesemwa mjini
hapana na Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha wa
Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernard Kibesse wakati akizungumza na
Wajasiriamali katika tukio la kukuza na kuendeleza Utalii la Lamadi
Utalii Festival, kwenye viwanja vya shule ya Itongo, mjini Lamadi.
Dkt. Kibesse alisema
licha ya kuwa Busega ni Wilaya mpya, wanabahati kupata Mkuu wa Wilaya
mwanamama na mchapa kazi kutokana na kubuni mambo mengi yenye kuleta
tija na fursa za kiuchumi DC Bi. Tan Mwera sambammba na Mkuu wa Mkoa
huo, Anthony Mtaka ambao wamekuwa na mbinu za kuja na fursa zenye
maendeleo.
Amnapo alieleza kuwa,
Lamadi itakuwa ikipokea Watalii wengi na kwa kuwa mwaka huu mradi huo
wa Disneyland unaanza kujengwa, Itakuwa inapokea Watalii zaidi ya 5,000
kwa mwaka ambapo itakuwa chachu katika kuingiza fedha za kigeni.
“Tunampongeza Mkuu
wetu wa Mkoa Anthony Mtaka na wasaidizi wake akiwemo DC Tano Mwera na
mwaka huu kituo cha Disneyland kinaanza kujengwa hapo eneo la pori la
akiba la Kijereshi.
Tupopamoja, tutumieni, tuambieni shida zenu tuwafikishie kwa Jemedali Rais, John Pombe Magufuli.
Na kwa kuwaambia tu,
Magufuli anaiependa sana Busega, kwani Mkuu wa Majeshi anatoka Busega,
Gavana anatoka Busega na wapo wengi wanaotoka Busega mmependelewa
kwelikweli, sasa suala sio kupendelewa, tuitumie hiyo nafasi tujiletee
maendeleo na kuliletea Taifa maendeleo kupitia Busega hii hii ambayo kwa
sasa ni mpya lakini itakuwa ni ya kitofauti hapo baadae.” alisema Dkt.
Kibesse.
Na kuongeza kuwa:
“Nchi zote za Ulaya, Asia, Afrika na kote, watakuwa wanakuja Tanzania,
lakini watakuwa wanakuja Busega na mtakuwa mnawaona hapa Lamadi.
Nilikuwa huko Marekani Mwezi wa Sita na wa Saba, watalii karibu 10,000
huwa wanaenda Florida na California kuangalia michezo ya maajabu ya
Disneyland hicho ambacho sasa kinakuja Afrika katika nchi ya Tanzania,
Mkoa wa Simiyu Wilaya ya Busega” alisema Dkt. Kibesse.
Pia aliongeza kuwa,
Wananchi wa Busega kwa kuwa hawapati fedha za kigeni za kutosha,
wametakiwa kutumia fursa za kuwekeza huduma za Kitalii nyingi katika mji
huo wa Lamadi.
“Tutumieni fursa za
kupata fedha za kigeni ‘Dolla’, sisi Lamadi hatuzipati sana Dolla,
fursa za mahoteli ni sasa na watakaopata ajira ni wana wa Lamadi,
tunakila sababu ya Busega kujidai”. alisema. Dkt. Kibesse.
Akielezea kwa kina
juu ya uchumi wa nchi, matukio kama matamasha na majukwaa ya kiuchumi
katika Utalii, kama ilivyo kwa Lamadi Utalii festival yanafanyika kwa
wakati muafaka kabisa kwa nchi kuhimiza ongezeko la fedha za kigeni na
Utalii ndio bidhaa inayoongoza kuingiza fedha za kigeni katika nchi hata
Wananchi na Rais wanatembea kwa kujidai kwa sababu nchi ina fedha za
kigeni za kutosha.
“Nimetoa mfano kwamba akiba iliyopo sasa hivi hata tukasema watanzania wote tukae hatuzalishi, jambo ambalo haliwezekani.
Hatuzalishi tumekaa
tu tunakula ‘bata’ tunakunja nne, tunakunywa zetu soda, kajuisi na
kamvinyo kidogo, tunauwezo wa kuimili mikiki yote na uagizaji wa bidhaa
kutoka nje kwa miezi sita.
Ebu fikiria hiyo
hali, kwamba nchi imelala haifanyi chochote, bado inaweza kuwa
‘fanctional’ kwa Miezi Sita, sasa hilo sio jambo dogo kwa sababu, moja
nchi haiwezi kulala, inaendelea kila siku. kwa hiyo naomba tutumie
matamatasha haya kuenzi Utalii wa ndani na kuvutia watalii wengi zaidi
na tytaingiza pesa za kigeni.” alisema Dkt. Kibesse.
Aidha, akizungumzia
juu ya uwepo wa benki chache kwenye mji huo wa Kiutalii, alisema kwa
muda mrefu Busega ilikuwa na benki moja tu ya Azania, ambayo ipo katika
mji wa Lamadi hivyo amewaomba wadau kuja kuekeza huduma hizo.
“Busega ni Wilaya mpya. benki nyingi huwa zipo kwenye miji na zikijitanua sana zinaenda kwenye Wilaya.
Busega imechelewa
sana ndio maana nilipoingia kwenye madaraka haya niliyopo niliizita
benki za Kizalendo za CRDB, NMB, POSTA, nikasema haiwezekani nyinyi
benki za kizalendo hampo Busega, wameahidi watakuja, kwani benki zikiwa
nyingi sehemu fulani ndio chocheo la uchumi hivyo nahimiza mabenki kuja
Lamadi ingawa NMB wameanza Nyanshimo.
Lamadi ndio kila kitu
maana nchi jirani wanapita hapa na mzunguko wa kibiashara hapa ni
mkubwa hivyo natumia wasaha huu mabenki yaje kuwekeza.” Alimalizia Dkt.
Kibesse.
No comments :
Post a Comment