
…………………………………………………………………………………………
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP Simon Sirro amesema Tanzania inanufaika kiulinzi na usalama kutokana
na kuwa mjumbe wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa nchi za ukanda wa
Kusini mwa Afrika (SARPCCO).
IGP Sirro ameyasema hayo leo
wakati alipokuwa akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kikao na
Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Polisi
Zimbabwe, TG Matanga ambaye yupo nchini kwa ziara maalum.
IGP Sirro amesema kuwa kutokana na
kuwa mjumbe wa shirikisho hilo, Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa
kuzuia na kudhibiti makosa yanayovuka mipaka yakiwemo makosa ya
usafirishaji haramu wa binadamu, wizi wa magari na dawa za kulevya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Shirikisho hilo ambaye pia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Zimbabwe, Kamishna
Jenerali TG Matanga, amesema yupo nchini kwa ziara maalum ya kufanya
tahmini ya utekelezaji wa maazimio ya INTERPOL pamoja na maazimio ya
SARPCCO.
No comments :
Post a Comment