Balozi wa Tanzania nchini Malaysia
Mhe Dkt. Ramadhani Kitwana Dau akimuonesha moja kati ya filamu ya
utalii Balozi wa Indonesia nchini Malaysia Mhe. Balozi Rusdi Kirana

Balozi wa Tanzania nchini Malaysia
Mhe. Dkt. Ramadhani Kitwana Dau akimkabidhi moja kati ya filamu za
utalii Balozi wa Indonesia nchini Malaysia Mhe Balozi Rusdi Kirana
…………………………………………………………………………………………….
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia
Mhe Dkt Ramadhani Kitwana Dau, ambaye pia
anawakilisha Indonesia
amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Indonesia nchini Malaysia
Mhe Rusdi Kirana na kukubaliana kutangaza fursa za utalii wa Tanzania.
Mara baada ya mazungumzo hayo,
Balozi Dau alipata fursa ya kumkabidhi Mhe Balozi Kirana filamu za
kutangaza utalii wa Tanzania ambapo filamu hizo zitaoneshwa kwenye ndege
bila malipo yoyote kutoka ya Serikali ya Tanzania.
Mhe Kirana ni mfanyabiashara
mkubwa anaemiliki Mashirika ya ndege ya Lions Group, Batik na Malindo.
Kwa pamoja, mashirika hayo yana ndege zaidi ya 300 na limeajiri
wafanyakazi 43,000.
Aidha mashirika hayo yanahudumia
abiria milioni 60 kwa Mwaka (wastani wa abiria 160,000 kwa Siku) na ina
Safari 3,400 za kwenda na kurudi kwa Siku. Mashirika hayo yanatoa Huduma
za Safari kwenye nchi zaidi ya 50 duniani.
Ubalozi wa Tanzania umemshawishi
na amekubali kutangaza utalii wa Tanzania kwenye ndege zake kupitia
inflight entertainment bure ambapo pamoja na mambo mengine filamu hizo
zitasaidia kutangaza fursa za utalii wa Tanzania.
Katika mazungumzo yao, Mabalozi
hao wamekubaliana umuhimu wa kutangaza utalii katika ukanda wa Kusini
Mashariki ya Asia ambapo Balozi Kirana ameahidi kuanzisha Safari za
ndege kwenda Tanzania baada ya kufanya mazungumzo na Mawakala wa utalii
wa Tanzania. Balozi huyo pia ameonesha utayari wake wa kukutana na
kujadiliana na mawakala wa utalii wa Tanzania kuhusu kuanzisha Safari za
ndege baina ya Indonesia na Tanzania. Mkutano huo Utafanyika mwezi
Februari 2020 katika Kongamano la Uwekezaji baina ya Tanzania na
Indoensia (Tanzania/Indoensia Investment Forum) litakalofanyika Jijini
Jakarta Indoensia tarehe 24-26 Septemba 2020.
Aidha katika mazungumzo hayo, Mhe
Dkt Dau alimwalika Mhe Balozi Kirana kutembelea Tanzania Mwaliko ambao
ameukubali na ameahidi kuja Tanzania katikati ya mwezi Septemba 2020.
kwa upande wake, Mhe Balozi Kirana amemkabidhi Mhe Balozi Dkt Dau mfano wa ndege zake kwa ajili ya kupamba ofisi.
No comments :
Post a Comment