Umati wa wakazi wa Jiji la Dar es
Salaam waliofurika katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, Dar es Salaam jana,
kushuhudia uzinduzi rasmi wa Kampeni usafi ya Omo Ng’arisha Festival
wakifuatilia matukio ya uzinduzi huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Unilever Tanzania, David Minja (wa nne kushoto), akikata utepe kuzindua
kampeni ya kitaifa ya usafi wa iliyopewa jina la Omo Ng’arisha Festival
katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam jana.

Wasichana wa promosheni wa
Kampeni ya Omo Ng’arisha festival, wakishika mifuko yenye sabuni za Omo
kunogesha uzinduzI rasmi wa kampeni ya miezi sita ya usafi iliyopewa
jina la Omo Ng’arisha Festival katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, jijini
Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Unilever Tanzania, David Minja, akizungumza na umati wa watu
uliojitokesa katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, Dar es Salaam jana
kushuhudia uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya usafi iliyopewa jina la
Omo Ng’arisha familia katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, jijini Dar es
Salaam.

Wakazi wa Jiji la Dar e Salaam
wakichangamkia kununua sabuni za Omo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya
Omo Ng’arisha Festival jijini humo jana.

Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam
akisikiliza maelezo kuhusu ubora wa sabuni ya Omo kutoka kwa wasichana
wa mauzo wa bidhaa hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Omo Ng’arisha
Festival jijini Dar es Salaam jana.

Hapa wakionyesha jinsi ya ufuaji
bora wa nguo kwa kutuma sabuni ya Omo ili kupata matokeo bora. Hapo ni
katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, Dar es Salaam kwenye wa Kampeni ya Omo
Ng’arisha Festival.

Balozi wa Kampeni ya Omo Ngarisha
Festival, msanii nguli wa muziki wa taarabu nchini Tanzania, Bi. Isha
Mashauzi akifanya vitu vyake wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini
Dar es Salaam jana.

Msani mahiri wa muziki wa singeli,
Seif Mwinjuma ‘Sholo Mwamba’ akikonga nyoyo za maelfu ya wakazi wa Jiji
la Dar es Salaam waliofurika katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, Dar es
Salaam jana kushuhudia uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Omo Ng’arisha
Festival.
…………………………………………………………………………………………….
KAMPUNI
ya bidhaa mbalimbali ya Unilever Tanzania imezindua kampeni maalumu ya
ya usafi miezi sita iitwayo ‘Omo Ng’arisha Festival’ itakayofanyika
Tanzania nzima ikiwa na lengo la kuhamasisha faida, ubora na matumizi
sahihi ya sabuni bora ya Omo..
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo
katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, Jiji la Dar es Salaam leo, Meneja
Msoko wa bidhaa ya Omo, Bi. Upendo Mkusa alisema ni matumaini yao
kwa
kupitia kampeni hiyo jamii itatambua matumizi sahihi ili kupata matokeo
yanayotarajiwa.
“Ni matumaini yetu watanzania
watatumia sabuni ya Omo kwa usahihi kutokana na ukweli kuwa Omo Fast
Action na Omo Extra Fresh ni bora katika kupambana na uchafu kwani ina
nguvu zaidi ya mara 10 kuliko sabuni za kawaida na ni ukweli kuwa
ukitumia Omo kufulia nguo za familia yako wewe na nguo za familia yako
mtang’aa, nguo zako ziking’aa wewe na familia yako mtang’aa, tunataka
kuona watanzania waking’aa,” alitanabaisha Bi. Upendo.
Akizungumza zaidi kuhusu kampeni
hiyo, Bi Upendo alisema mara baada ya uzinduzi huo, kampeni hiyo
itaendelea kwa matamasha na matukio mengine katika mikoa ya Dodoma, Dar,
Mwanza, Arusha, Moshi na Mbeya. Kuifanya kampeni hii kuwa yenye
bashasha na mvuto, Unilever imemtangaza Msanii maarufu nchini Tanzania,
Bi. Isha Mashauzi kuwa Balozi wa Kampeni ya Omo Ng’arisha,
atakayeshiriki katika matukio mbalimbali katika kampeni hii ikiwemo
michezo, michezo ya kufurahisha na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii
mbalimbali.
Kampeni itashirikisha timu ya
promosheni ya Omo kwa kupita mlango kwa mlango majumbani, kwenye maeneo
ya wazi na katika sehemu za biashara kuijulisha jamii juu ya ubora,
faida na matumizi sahihi ya OMO, ambayo ni moja ya bidhaa kubwa zaidi ya
Unilever.
Pamoja na hayo meneja huyo alisema
kwa kutambua na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika
kuendeleza uchumi wa viwanda na katika kuwaletea watu wake maendeleo,
wameandaa zoezi maalumu la kuwatambua Wanawake Wajasiriamali 10 Bora
katika kila mkoa watakapofanya kampeni hiyo na kuwapa zawadi
itakayowasaidia kuboresha biashara zao hivyo kuwafanya kung’aa.
“Ni imani yetu wanawake hawa
miogoni mwao kuna wenye biashara ndogondogo, tutawatambua na kuwapa
zawadi. Ni matarajio yetu utambuzi huu utaleta tija na kuwa kichocheo
katika utendaji wao hivyo kukuza biashara zao.
“Unilever pia tupo mstari wa
mbele katika kusaidia jamii, ni katika muskabali huo timu yetu ya
kampeni katika mikoa hiyo niliyoitaja, tutatembelea katika mahospitali
ambako tutaonyesha moyo wa kujali kwa kutoa msaada wa sabuni za Omo kwa
wagonjwa waliolazwa katika hospitali hizo tukiongozwa na balozi wetu wa
Omo Bi. Isha Mashauzi.
“Unilever pia tunaunga mkono
juhudi za serikali katika kuwataka wananchi kufanya usafi wa mazingira
yao, na nina furaha kwamba kupitia kampeni ya Omo Ng’arisha katika kila
mkoa timu yetu ya Omo Ng’arisha familia itashiriki katika shughuli za
usafi kwa kushirikiana na viongozi wa mkoa huo,” aliongeza Bi. Upendo.
Aidha Meneja Masoko huyo
alisema Unilever inatoa shukurani kubwa kwa ushirikiano inaoupata kutoka
mamlaka mbalimbali za kibiashara na kiserikali hapa nchini.
“Tunaipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kuweka mazingira wezeshi na
juhudi yake katika kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zinazokabili
jumuiya ya wafanyabiashara. Kwa upande wetu tunaahidi kuongeza ubora wa
bidhaa zetu kuhakikisha zinakidhi mahitaji ya wateja wetu, tukifanya
biashara kwa kuzingatia kanuni na taratibu zote zilizopo huku
tukiangalia namna bora zaidi ya kuinufaisha jamii ya watanzania,”
alisema.
Licha ya bidhaa ya Omo ikiwa na
aina mbili za Omo Fast Action na Omo Extra Fresh yenye nguvu mara kumi
zaidi, Unilever inazo bidhaa nyingine kama; Sunlight-sabuni ya unga,
inayotakatisha vizuri, yenye manukato na kulainisha ngozi, mafuta ya
mgando na losheni ya Vaseline yenye uwezo wa kutunza ngozi, Vim-sabuni
ya kusafishia ambayo ni kiboko ya uchafu wa nyumbani, AXE-sprei ya
mwili kwa wanaume inayokuacha na harufu nzuri kwa zaidi ya masaa 48 na
Royco mchuzi mix, kiungo cha chakula chenye viungo asilia 16 kwa
kuongeza ladha murua ya chakula.
No comments :
Post a Comment