Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisalimiana na
wanawake wa vikundi vya DARE na Ulonge vinavyojishughulisha na ujenzi
wa barabara na madaraja madogo wilayani Ludewa mkoai Njombe katika ziara
yake mkoani humo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifurahia mara
baada ya kupokea zawadi ya jogoo kutoka kwa kikundi cha vikundi vya DARE
na Ulonge vinavyojishughulisha na ujenzi wa barabra na madaraja madogo
wilayani Ludewa mkoani Njombe katika ziara yake mkoani humo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile( mwenye shati la
njano na kijani) akiwa katika picha ya pamoja vikundi vya DARE na
Ulonge vinavyojishughulisha na ujenzi wa barabra na madaraja madogo
wilayani Ludewa mkoani Njombe katika ziara yake mkoani humo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akishindilia
zege katika katika daraja dogo linalojengwa katika barabara ya lwilo
mbongo na wanawake na vijana wa vikundi vya DARE na Ulonge wilayani
Ludewa mkoani Njombe katika ziara yake mkoani humo.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
***************************
Na Mwandishi Wetu Ludewa Njombe
Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amewtaka wanawake na
vijana nchini kutumia changamoto zilizopo katika maneo yao kama fursa ya
kujiajiri na kuajiri watu wengine.
Dkt.
Ndugulile ameyasema hayo wilayani Ludewa mkoani Nombe wakati
alipotembeela vikundi kazi vya wanawake na vijana vinavyojishughulisha
na kutengeneza barabara na madaraja madogo wilayani humo.
Dkt.Ndugulile
ameongeza kuwa vijana na wanawake wengi wamekuwa wakilalamika kukosa
ajira hasa kwa walimaliza elimu ya juu ila wanawake na vijana wa wilaya
ya Ludewa wamedhubutu kuchangamkia fursa ya kutengeneza barabara na
madaraja madogo.
“Sijawahi
kuona kitu kama hiki tangu nianze ziara zangu katika mikoa na wilaya
hongereni mmedhubutu na mkaamua ktuia fursa hii kupatakujiajir ni mwanzo
mzuri mtafika mbali” alisisitiza Dkt. Ndugulile.
Ameogeza kuwa
jambo linalofanywa na vikundi hivyo linaendana moja kwa moja na dhana
ya Maendeleo ya Jamii ya wananchi kushiriki katika shughuli za
kimaendeleo katika maneo yao kwa kuamsha ari yao katika kushiriki
shughuli hizo pamoja na kujiongezea kipato.
Aidha Dkt.
Ndugulile amezitaka Hlmashauri nchini kuhimiza wanawake na vijana
kujiunga katika vikundi vya kijasiriamali ili kuwawesha kupata mikopo
ya kufanya biashara na miradi mbalimbali kama wanavyofanya wanawake na
vijana wa wilaya ya Ludewa.
Dkt. Nduguile
amewapa moyo wanawake na vijana hao wa wilaya ya Ludewa katika harakati
za kutafuta kazi na kuwasihi vijana na wanawake wengine kutojibweteka
wakisubiri ajira za kujiajiri bali wajiongeze na kujiajiri na hata
kuajiri watu wengine.
“Jambo hili
mnalofanya ni jambo jema la msingi litawasaidia kupata kipato na kujinua
kiuchumi kwani kwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe.Rais
Magufuli inasisitiza watu kufanya kazi hasa vijana na wanawake” alisema
Dkt. Ndugulile
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Kikundi cha DARE Bi. Theopista Mhagama amesema kuwa
jumla ya vikundi 54 vimefanikiwa kujisajili katika Mamlaka mbalimbali
ambazo zitawawezesha kuomba na kupata kazi za kutengeneza barabara na
madaraja wilayani humo na Tanzania kwa ujumla
“Kwakweli
tunafarijika sana kwani tumeamua kwa dhati kujikwamua kiuchumi na sio
kukaa na kulalamika na kusbiri kufanyiwa kila kitu na Serikali wakati
kama vijana na wanawake tunaweza kufanya kazi tukajiajiri na kuajiri
wengine” alisema Bi. Theopista.
Ameongeza
kuwa mpaka sasa wamepata kandarasi ya kujenga madaraja madogo katika
barabara ya lwilo mbongo na yamefika katika asilimia 75 na wamedhutu
kuomba tenda za ujenzi wa barabara na madaraja za kitaifa kwani
wanakidhi vigezo kama wakandarasi wengine.
No comments :
Post a Comment