Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akiweka jiwe la msingi la Huduma za Mama na Mtoto, Bambi mkoani Kusini
Unguja. Januari 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akiangalia kitanda cha wazazi, baada ya kuweka jiwe la msingi la Huduma
za Mama na Mtoto, Bambi mkoani Kusini Unguja. Januari 17, 2020. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akiwahutubia wananchi, baada ya kuweka jiwe la msingi la Huduma za Mama
na Mtoto, Bambi mkoani Kusini Unguja. Januari 17, 2020. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akikagua maendeleo ya ujenzi wa maabara ya sayansi ya shule ya sekondari
Bwejuu, katika Mkoa wa Kusini Unguja. Januari 17, 2020. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akiwapa kasa chakula,kwenye bwawa la kufugia kasa, wakati alipokagua
miradi ya jamii katika kilimo cha kisasa, kwa wakulima wa Jozani, mkoani
Kusini Unguja. Januari 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akimshika kobe, wanaohifadhiwa katika hifadhi ya Jozani, mkoani Kusini
Unguja. Januari 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
*****************************
Na Maryam Kidiko .
Waziri mkuu
wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe, Kassim Majaliwa amewataka
Viongozi wa Serikali kuwatumikia wananchi bila ya ubaguzi na
kuhakikisha wanapata huduma muhimu za kijamii ili kutatua changamoto
zinazowakabili.
Hayo
ameyasema alipokuwa akizungumza na Viongozi mbali mbali wakati akifanya
ziara za kuangalia miradi ya maendeleo ikiwemo kuzindua Jengo la
huduma za Mama na Mtoto Bambi . .
Amesema kila
mtumishi wa umma ahakikishe anafanya kazi kwa vitendo na kuwajibika
kutokana na majukumu waliopangiwa ili kuhakikisha wananchi wanapata haki
zao za msingi.
Waziri Kassim
ameitaka Serikali ya mkoa wa kusini Unguja kuweka mpango mkakati wa
kuwafatilia wananchi wao katika vijiji vyao ili kujua changamoto
zinazowakabili na kuzitatua kwa haraka.
Amesema kuwa
Viongozi lazima waweke mpango mkakati wa kukuza uchumi na huduma za
kijamii zikiwemo skuli ,vituo vya afya ,kilimo na kukuza utalii nchini
ili taifa liweze kuingiza fedha za kigeni zitakazowasaidia wananchi
katika huduma muhimu.
Hata hivyo
amesema katika swala la usalama Serikali ihakikishe inaweka usalama wa
kutosha wa kulinda raiya na nchi kwa jumla ili kuwepo na amani na
utulivu.
Akitoa
Taatifa fupi ya Mkoa Mkuu wa Mkoa wa kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmuod
amesema kwa upande wa mkoa huo umejipanga kuhakikisha unatatua na
kushughulikia changamoto zote walizokuwa nazo wananchi .
Ziara hiyo ya
siku moja imetembelea miradi mitano ya kimaendeleo ikiwemo kuzindua
kituo cha afya ya kijiji kizimkazi Dimbani , ukaguzi wa maabara ya
sayansi Bwejuu,kukagua kilimo cha kisasa jozani na kuzindua huduma ya
mama na mtoto Bambi.
No comments :
Post a Comment