Mkuu wa Wilaya ya Kinondo ,Mhe.
Daniel Chongolo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa
zoezi la ulipaji kodi za majengo, kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri
hiyo Ndugu. Aron Kagurumjuli na kushoto ni Meneja wa TRA Mkoa wa
Kinondoni Bwana Masawe Masaka.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni, Ndugu. Aron Kagurumjuli akizungumza na waandishi
wa habari kuhusu kuanza kwa zoezi la ulipaji wa kodi za majengo,
katikati mwenyesuti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondo ,Mhe. Daniel
Chongolo.
********************************
Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni leo imezindua zoezi la uhamasishaji wananchi kulipa
kodi ya
majengo kwa kipindi cha mwaka 2019 / 2020 kitakacho malizika Juni 30
mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesema kuwa kwa
kipindi cha mwaka huu wa fedha wananchi wengi bado hawaja hamasika vya
kutosha kwenda kulipa kodi hiyo na kwamba iwapo watachelewa
watalazimika kulipa na riba.
Mhe. Chongolo amesema kuwa Rais
Dk. John Pombe Magufuli alipokutana na viongozi wa juu kutoka Mamlaka ya
Mapato Tanzania TRA mwakajana alitoa maelekezo na hivyo kushusha
kiwango cha tozo hiyo ambapo mwananchi mwenyenyumba ya kawaida atalipa
kiasi cha shilingi 10,000 huku mwenyenyumba ya Ghorofa kiasi cha
shingili 50,000.
Mhe. Chongolo amefafanua kuwa “
kwa wale wenye nyumba za Ghorofa wanalipa kiasi cha shilingi 50,000 kwa
floo, kama zipo floo 10 maana yake analipa shilingi 500,000, kama zipo
20 inamana atalipa shilingi 1,000,000, kwa hiyo unaweza kuona“ kodi hii
imeshuka kwa kiwango ambacho hakuna mwanachi ambaye hataweza kuilipia”
amefafanua.
Aidha Mhe. Chongolo ameeleza kuwa
Wilaya ya Kinondoni inajumla ya kaya zaidi ya 340,000 na kwamba iwapo
kila kaya italipa kodi hiyo itakuwa imekusanya kiasi cha zaidi ya
shilingi Bilioni 3.5 pesa ambazo zinaweza kutumika kwa ajili ya
kupeleka huduma kwa wananchi ikiwemo barabara, miundombinu ya maji
pamoja na huduma nyingine za msingi.
Hata hivyo Mhe. Chongolo
amesisitiza kuwa hadi kufikia Juni 30 mwaka huu asilimia 100 ya wakazi
wa Kinondoni wawe wameshalipa kodi hiyo na kwamba taarifa hiyo
itapelekwa kila Kata kwa ajili ya kuhamasisha wananchi wengi huku
wakifuatilia wale waliokuwa na malimbikizo ya madeni ya nyuma.
“ Niwasisitize wananchi wa
Kinondoni, wakati ni sasa na kwamba kama utakiuka sheria hii kuna hatari
ya kupoteza jengo lako, tuache tabia ya kusubiria tarahe za mwisho kama
ambavyo watu walifanya kwenye usajili wa laini za simu kwa kutumia
alama za vidole, niwasihi anzeni kulipa sasa” amesisitiza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo, Ndugu. Aron Kagurumjuli amesema kuwa lengo la Serikali
ni kukusanya mapato ya kutosha ili iwe na uwezo mkubwa wa kuwahudumia
wananchi na hivyo kuwasisitiza wakazi hao kujitokeza kulipa bila
kusubiri tarehe za mwisho.
Amefafanua kuwa “awali Halmashauri
ilikuwa ikikusanya kodi ya majengo kabla ya kuhamishiwa TRA, ila bado
lengo la Serikali ni lile lile la kukusanya mapato na ndio mana na mimi
niko hapa, kwa sababu Halmashauri na TRA hakuna tofauti bado ni Serikali
ile ile yenye lengo moja la kuwahudumia na kuboresha huduma za
wananchi.
Naye Meneja wa TRA Mkoa wa
Kinondoni Masawe Masaka amewataka wananchi kuchangamkia fursa
iliyotolewa na Rais Dk. Magufuli yakulipa kodi hiyo na kwamba wasisubiri
kulipishwa faini pindi watakapo shindwa kulipa kwa wakati.
No comments :
Post a Comment