******************************
Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dkt. Hussein mwinyi
amesema Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani
kwenye mataifa yenye machafuko kwa
kupeleka vikosi vyenye uwezo wa hali
ya juu ili kuhakikisha amani inatawala duniani.
Ameyasema hayo leo jijini Dar
es salaam katika hafla ya upokezi wa vifaa vya kijeshi vinavyotumika
katika mchakato wa kulinda amani vilivyotolewa na Serikali ya Marekani.
Akizungumza katika hafla hiyo
Dkt.Mwinyi amesema kuwa nchi ya Tanzania na Marekani zimekuwa na
ushirikiano wa karibu kupitia majeshi pamoja sekta mbalimbali ikiwemo
maswala ya kijamii,uchumi na elimu.
“Msaada huo utasaidia kuongeza
uwezo wa vikosi maalumu vya kulinda amani katika kukabiliana na
changamoto za kulinda amani duniani ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa
kukabiliana na majanga ya dharula yanayotekea hapa nchini na kuongeza
thamani ya jeshi”.Amesema Dkt.Mwinyi.
Kwa upande wake Kaimu Balozi
wa Marekani hapa nchini Bw. Inm Patterson amesema kwa takribani mwaka
mmoja vikosi vya Tanzania vimeweza kupatiwa mafunzo ya kuviendesha na
kuvitumia vifaa hivyo, hivyo ni jukumu lao jeshi kuvitunza na kuweza
kusaidia wananchi katika majanga mbalimbali na kuendelea kurfanya
mazoezi ili kuweza kukabiliana na jambo lolote linaloweza kujitokeza.
Pamoja na hayo Mkuu wa majeshi
ya ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo amesema kuwa vifaa hivyo
walivyokabidhiwa na Marekani ni kuunga mkono jitahada za jeshi la
Tanzania katika kulinda amani na vitasaidia vikundi vya jeshi kutoa
msaada wa haraka kwa wenye uhitaji.
Aidha vifaa vilivyokabidhiwa
leo katika hafla hiyo ni pamoja na magari,jenereta,jiko maalumu,mashine
ya kusafishia maji vyenye jumla ya thamani ya dollar millioni 18.
No comments :
Post a Comment