Waziri wa Madini Doto Biteko
katikati akiwa na Waziri wa Nishati Merdad Kalemani kulia na Mkuu wa
Wilaya ya Chato Mhandisi Charles Kabeho wakiweka sahihi mara baada ya
kuwasiri katika ufunguzi wa Soko Kuu la Madini Chato
Waziri wa Madini Doto Biteko
wakwanza kushoto, anaefata Waziri wa Nishati Merdad Kalemani, wakwanza
kulia ni Rais wa FEMATA Jonh Bina wakiwa na baadhi ya wadou wa madini
wakifungua jiwe la msingi la Soko Kuu la Dhahabu Chato.
Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kwenye ufunguzi wa Soko la Madini Chato
Rais wa Shirikisho la Wachimbaji
Wadogo Nchini (FEMATA), John Bina akizungumza na wadau wa madini katika
ufunguzi wa Soko la Madini Chato
Waziri wa Madini Doto Biteko
kwapili kusho, atikati Waziri wa Nishati Merdad Kalemani kushoto, Mkuu
wa Wilaya ya Chato nyuma kushoto, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita
Daniel Mapunda wakitoka eneo la Soko la Madini Chato mara baada ya
Ufunguzi.
Waziri wa Madini Doto Biteko
kulia akiwa na Mwalimu wa aliyewahi kumfundisha Somo la Kemia ambaye pia
ni Mwalimu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli
…………………………………………………..
Na Tito Mselem, Chato
Tangu kuanzishwa kwa masoko ya
madini nchini, Mkoa wa Geita umeongeza ukusanyaji wa mapato kwenye Sekta
ya Madini kutoka chini ya bilioni 1 kwa mwaka mpaka kufikia zaidi ya
billion 3.5 kwa mwaka.
Hayo yameelezwa na Waziri wa
Madini Doto Biteko, alipokuwa akifungua Soko Kuu la Madini ya dhahabu
Chato lililopo Buseresere Mkoani Geita na kwamba, soko hilo limefikisha
idadi ya
masoko 29 nchini na masoko 8 yaliyofunguliwa Mkoani
Geita ambalo kwa sasa lina ofisi 10 za Madalali (Brokers) wanao nunua
madini hayo.
Aidha, Waziri Biteko amewataka
maafisa wa Serikali kutowasumbua wachimbaji na wafanyabiashara wa madini
pindi wanapopeleka madini yao sokoni na mchimbaji au mfanyabiashaya
yoyote wa madini haruhusiwi kukaa na madini nyumbani kwake bila ya kuwa
na nyaraka kutoka serikalini.
“Kipindi cha nyuma serikali
ilikuwa inatoa leseni kwa wafanyabiashara bila kujua wananunua wapi wala
wanauza wapi ila leo wanunuzi wanajua wakanunue wapi na wakauze wapi,,
haya ni mafanikio makubwa sana kwenye Sekta ya Madini na anae stahili
pongezi si Wizara ya Madini wala si Doto Biteko bali ni Rais mwenyewe
Dkt. John Pombe Magufuli na wadau wa madini kwa kukubali kufuata
sheria”, alisema Waziri Biteko.
Wakati huo huo, Waziri Biteko
amewataka Wachimbaji na wafanyabiashara wa Mkoa wa Geita kufanya
shughuli ya madini kwa kufuata sheria, kuepuka ukwepaji wa kodi na
kutunza kumbukumbu ili kuepuka usumbufu usio wa lazima.
“Wilaya ya Chato ina jumla ya
leseni za uchimbaji mdogo 276 ambapo ni yatatu baada ya Wilaya ya Geita
yenye jumla ya leseni 630 na yapili ni Bukombe yenye jumla ya leseni 376
za uchimbaji mdogo wa madini,” alisema Waziri Biteko.
Imeelezwa kuwa, Mwaka 2017
kulifanyika Marekebisho ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 ikiwa ni
jitihada ya Serikali kudhibiti utoroshwaji wa madini nchini ambapo,
kifungu cha 27C (1 na 2) cha Marekebisho ya Sheria ya Madini kinaelekeza
uanzishwaji wa Masoko ya Madini ambayo yana faida kubwa kwa wachimbaji,
wafanyabiashara wa madini na Serikali kwa ujumla.
Kwa upande wake, Mbunge wa Chato
ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Merdad Kalemani amempongeza Waziri
Biteko kwa kazi nzuri anazozifanya na kueleza kuwa pamoja na maelekezo
mazuri wanayo yapata kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli, Wizara ya Madini imejipanga kuhakikisha
inasimamia Sekta ya Madini kikamilifu na imeongeza pato la Nchi kwa
kiwango kikubwa.
“Tulililia sana Soko la
Madini Chato, lakini leo tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kilio chetu
kimepata majibu,” alisema Dkt. Kalemani.
Nae, Rais wa Shirikisho la
Wachimbaji Wadogo Nchini (FEMATA), John Bina amemuomba Waziri Biteko
kuendelea kuwapa wachimbaji wadogo maeneo ya kuchimba na kaipongeza
serikali kwa kugawa Transfoma saba kwa wachimbaji wadogo kila Mkoa.
No comments :
Post a Comment