Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb)
……………………………………………
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo – Sumbawanga
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga (Mb) ameliagiza jeshi la Polisi nchini kumkamata na kumfungulia
mashtaka ya uhujumu uchumi Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa
Rukwa Anosisye Mbetwa.
Waziri Hasunga ametoa agizo hilo
jana tarehe 28 Disemba 2019 wakati akizungumza kwenye
kikao cha kazi
kilichowakutanisha viongozi na wanachama wa vyama vya ushirika (AMCOS)
katika ukumbi wa mikutano kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Mrajis huyo ameweka kizuizini kwa
kubainika kushiriki kuingia mkataba na Kampuni ya kusambaza mbolea ya
ELI AGROVENT CO kinyume na taratibu za serikali hali iliyopelekea chama
kikuu cha ushirika mkoani humo Ufipa Cooperative Union (UCU) kutapeliwa
shilingi Milioni 277 huku wanachama wake wakiendelea kuhangaika juu ya
upatikanaji wa mbolea.
Miongoni mwa vipengele vya
Mkataba huo ulioingiwa tarehe 22.11.2019 vinasema kuwa Kampuni hiyo
itamuuzia UCU mbolea ya Tani 1,901.05 yenye thamani ya shilingi Bilioni
2,384,266,812 ambapo bei ya mbolea hiyo iko juu ukilinganisha na
maelekezo ya serikali juu ya bei elekezi za mbolea nchini.
Hadi kufikia tarehe 3.4.2020
chama hicho kinatakiwa kiwe kimekamilisha malipo hayo huku mkataba
ukionesha kuwa malipo hayo yanasimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa
asilimia 100 jambo ambalo Ofisi ya Mkoa haifahamu.
Waziri Hasunga alisema kuwa lengo
la kuanzishwa vyama vikuu vya ushirika katika mikoa ni kuweza kusaidia
kuagiza pembejeo kwa niaba ya wanachama ili gharama za mbolea na hivyo
kuushangaa mkoa wa Rukwa kwa kukubali kuingia mkataba wa kuuziwa mbolea
ambayo bei yake ipo juu na kufafanua kuwa bei kubwa ya mbolea inatokana
na gharama za usafirishaji gharama za faida kutoka bandarini kuja huku
na kuongeza kuwa kuona manufaa ya ushirika bei ya ushirika inatakiwa iwe
chini ya bei za soko ambazo wanauza wafanyabiashara kwenye masoko.
“Tulisema vyama vya ushirika
visaidie kuagiza pembejeo kwa niaba ya wanachama ili gharama za mbolea
zishuke hivi hapo kwenu huku rukwa ndio zimeshuka hapo yaani bei
mnapeleka mbele ndio mnasema imeshuka halafu mnasema watu wawe na imani
na hivyo vyama haiwezekani bei kubwa ya mbolea inatokana na gharama za
usafirishaji gharama za faida kutoka bandarini kuja huku bei ya ushirika
inatakiwa iwe chini ya bei za soko” Alikaririwa Mhe Hasunga na kuongeza
kuwa
“Bei za soko ambazo wanauza
wafanyabiashara kule kwenye masoko ziwe juu za kwenu ziwe chini ndio
mtasema ushirika una manufaa ushirika gani unakwenda kuuza bei ya juu
ambayo sio sawa na soko, utakuwa na akili timamu wewe utoe hela yako
ukanunue bei ya juu wakati ungenunua kwa shilingi 54000 ungebaki na hela
ya kwenda kumnunulia mtoto daftari”
Kadhalika, Mhe Hasunga ameagiza
kukamatwa na kufunguliwa kesi ya uhujumu Uchumi Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya kusambaza mbolea ya ELI AGROVENT CO Bw Elias Ndomba kutokana
na kuwauzia wakulima mbolea kinyume na bei elekezi ya serikali
iliyotangazwa hivi karibuni.
No comments :
Post a Comment