Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na Katibu Tawala Mkoa
wa Tabora Msalika Makungu (wa tatu kutoka kulia) na viongozi wengine
katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo mafupi
kwenye Ofisi ya Mhkuu wa Mkoa wa Tabora wakati ziara yake ya kikazi
mkoani humo leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (kushoto) akizungumza na wafanyakazi
waliopo chini ya Wizara ya Maliasi na Utalii(hapo kwenye picha) leo
wakati wa ziara yake mkoani Tabora. Kulia ni Kaimu Meneja wa Wakala wa
Huduma za Mistu Tanzania Kanda ya Magharibi Thomas Wambura.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (kushoto) akizungumza na wafanyakazi
waliopo chini ya Wizara ya Maliasi na Utalii(kulia) leo wakati wa ziara
yake mkoani Tabora.
*******************************
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameitaka Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania (TFS) kuhakikisha inawekeza katika mistu yao ili kuwa na vyanzo
endelevu vya ukusanyaji mapato badala ya kusubiri watu wakosee ndipo
wakusanye mapato.
Alisema hatua ya kutegemea
kukusanya mapato yanatokana na adhabu kwa waharifu na
wanakamatwa na
mkaa katika vizuizi hakuwezi kuwafanya kuwa na mapato endelevu.
Kanyasu alitoa kauli hiyo leo
Mkoani Tabora wakati akizungumza na wafanyakazi walio chini ya Wizara ya
wa Maliasili na Utalii kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa TFS.
Alisema wakati umefika kwa TFS
kuwekeza katika msitu yake kwa upandaji wa miti na ufugaji wa nyuki ili
kuwawezesha kuwa na vyanzo vya mapato badala ya kusubiri watu wafanye
makosa ndio wapate mapato kupitia adhabu wanapatia.
Kanyasu aliongeza kuwa ipo siku
watu wanaoharibu mistu watastarabika na kuacha makosa kama vile kukata
miti na kuacha kuchoma mkaa bila vibali na hivyo kujikuta hawana vyanzo
vya mapato.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri
huyo ameutaka uongozi wa Mkoa wa Tabora kuharakisha mchakato wa
kuikabidhi uendeshaji wa bustani ya wanyama pori(zoo) iliyopo Manispaa
ya Tabora kwa Wizara ya Maliasili na Utalii ili iweze kuiendesha kwa
faida na hivyo kusaidia katika kuingizia Serikali mapato.
Alisema uboreshaji wa bustani hiyo
ni muhimu sana kwa Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kuwaongezea kuongeza
idadi ya watalii na kipato cha Mkoa huo na wakazi wake.
Kanyasu alisema badala ya watalii
kwenda moja kwa moja katika vivutio vingine wanaweza kuaniza kwa
kutembelea bustani hiyo na hivyo watu wenye Hoteli, Mkoa na wenyeji
kujipata kipato kupitia tozo mbalimbali wanazolipa wageni.
Aidha alisema kuwa Wizara yake
imekuwa ikilipa Maaskari wanaolinda bustani hiyo wakati bado haijatumika
ipasavyo kuiingizia Serikali mapato na kuongeza kuwa kama Mkoa unaona
eneo hilo litumike kwa shughuli nyingine wawaeleza ili wanyama waliomo
warudishwe porini na walinzi wapelekwe maeneo mengine yenye upungufu
watumishi wa kada hiyo.
Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa
wa Tabora Msalika Makungu alisema suala hilo tayari Kamati inaendelea
kulifanyia kazi na ndani ya siku chache watalipatia ufumbuzi kwa maslahi
ya pande zote.
No comments :
Post a Comment