Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango amewaagiza wataalamu wa
mipango nchini kutoa mapendekezo ya kibunifu ambayo yataiwezesha nchi
kunufaika na utaratibu wa ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi
(PPP).
Agizo
hilo amelitoa wakati akifungua Kongamano la Wanamipango kwa mwaka 2019
lililofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini
Dodoma.
Alisema
kuwa bado kunachangamoto ya utekelezaji wa PPP nchini na kuwataka
wataalamu hao kujadili ili kuona wapi nchi imekosea na kutoa suluhu ya
namna ya kutatua changamoto hizo.
“Lakini
PPP niliyoona imefanikiwa sana ni kwenye sekta za kijamii, najua
tumefanya vizuri kwenye huduma za afya na elimu, lakini kweye miradi ya
miundombinu bado”, alibainisha.
Aidha,
Dkt. Mpango aliwagiza wataalamu hao kujadili namna bora ya kutanua wigo
wa kukusanya kodi ili kuiwezesha nchi kuweza kujiendesha pamoja na
kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.
Alisema
katika suala la kodi, ukusanyaji kodi bado kuna shida kwani hata idadi
ya walipakodi ni ndogo ukilinganisha na idadi ya wananchi.
Aliwataka
wataalam hao kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji mapato ya Serikali na
kuhakikisha yanatumika vema ili kuweza kukuza uchumi wa nchi.
Aliseme
ni vema wataalam hao wakatambua kuwa katika harakati za kuiwezesha nchi
kuwa ya uchumi wa kati ni wazi baadhi ya vyanzo vya ugharamiaji wa
miradi vitapungua hivyo ni lazima nchi iweke mipango madhubuti ya
kutafuta rasimali kutoka katika vyanzo mbadala vya mapato za kuweza
kugharamia miradi hiyo.
Waziri
Mpango alisema kwa kuwa Kongamano hilo linalenga kujadili namna ya
kugharamia maendeleo, ni vema wataalamu hao wakajadili na kujatoa
muongozo wa namna Tanzania itakavyoweza kuvutia wawekezaji binafsi kwa
wingi.
“Ni
matarajio ya Serikali kongamano hili litajadili wawekezaji ambao
watafanya uwekezaji utakao inufaisha nchi na wao wenyewe, yaani
uwekezaji huu uwe ni win-win”, alifafanua.
Aidha,
Dkt. Mpango aliwaagiza wataalam hao kujadili namna majukumu ya benki za
ndani katika kugharamia miradi ya maendeleo ili kuona namna ya
kuzishirikisha katika miradi hiyo.
Naye
Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Lorah Madete alisema
kuwa kupitia kongamano hilo washiriki watapata fursa ya kujadili
mawasilisho yatakayoendana na dhima ya kongamano ikiwemo Vyanzo bunifu
vya ugharamiaji wa mipango ya maendeleo ya Taifa, Sera, Sheri ana
Kanuni.
Kongamano
hilo la siku mbili limekutanisha wataalamu wanaohusika na masuala ya
mipango kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali,
Taasisi, Sekretariaeti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Sekta
Binafsi.
No comments :
Post a Comment