Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga
Mohammed Kahundi amezindua zoezi la Upuliziaji wa Viua Dudu
‘Larviciding’ katika mazalia ya mbu mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya
mikakati ya kupambana na ugonjwa wa malaria nchini ili kutekeleza kauli
mbiu ya ‘Ziro Malaria inaanza na mimi’.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga
Mohammed Kahundi (mwenye suti nyeusi) akizindua zoezi la Upuliziaji wa
Viua Dudu ‘Larviciding’ katika mazalia ya mbu mkoa wa Shinyanga kwa
kupulizia dawa ya viua dudu katika bwawa la Shunu lililopo katika
Halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji leo Jumamosi Desemba 21,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga
Mohammed Kahundi (mwenye suti nyeusi) akiendesha zoezi la Upuliziaji wa
Viua Dudu ‘Larviciding’ katika bwawa la Shunu lililopo katika
Halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji.
Kaimu
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi (katikati) akichota
maji katika bwawa la Shunu lililopo katika Halmashauri ya wilaya ya
Kahama Mji ili kuangalia aina na idadi ya viluilui vilivyopo kwenye
bwawa la maji.
Kaimu
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi na wadau mbalimbali wa
afya wakiwa katika bwawa la Shunu wakati wa kuzindua zoezi la Upuliziaji wa Viua Dudu ‘Larviciding’ katika mazalia ya mbu mkoa wa Shinyanga.
Awali Afisa Afya halmashauri ya Ushetu Genoveva Gabriel akitoa ufafanuzi namna ya kuendesha zoezi la Upuliziaji wa Viua Dudu ‘Larviciding’ katika mazalia ya mbu.
Mhudumu wa afya ngazi ya jamii kutoka kata ya Ulewe,Brown Christian akiendelea na zoezi la Upuliziaji wa Viua Dudu ‘Larviciding’ katika bwawa la Shunu.
Kulia ni Meneja Mradi wa Badilisha Tabia
Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T- MARC, Hamid Al- Alawy akimweleza
jambo Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi wakati wa
uzinduzi wa zoezi la Upuliziaji wa Viua Dudu ‘Larviciding’ katika
mazalia ya mbu mkoa wa Shinyanga kwa kupulizia dawa ya viua dudu katika
bwawa la Shunu lililopo katika Halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji.Wa
kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi akizungumza
wakati wa uzinduzi wa zoezi la Upuliziaji wa Viua Dudu ‘Larviciding’
katika mazalia ya mbu mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga
Mohammed Kahundi akiondoka katika bwawa la Shunu baada ya kuzindua zoezi
la Upuliziaji wa Viua Dudu ‘Larviciding’ katika mazalia ya mbu mkoa wa
Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga
Mohammed Kahundi na wadau wa afya wakiondoka katika bwawa la Shunu baada
ya uzinduzi wa zoezi la Upuliziaji wa Viua Dudu ‘Larviciding’ katika
mazalia ya mbu mkoa wa Shinyanga.
Awali Kaimu Katibu Tawala mkoa wa
Shinyanga Mohammed Kahundi akizungumza na watoa huduma za afya ngazi ya
jamii na wadau wa afya katika Ukumbi wa Kahama Super Logde Mjini Kahama.
Kahundi alisisitiza elimu kuhusu udhibiti wa ugonjwa wa malaria
iendelee kutolewa kwa njia mbalimbali zikiwemo wahudumu wa Afya ngazi ya
Jamii, Vituo vya afya, katika kaya na kwa njia ya vyombo vya habari.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga
Mohammed Kahundi akielezea mikakati inayotumika mkoani Shinyanga
kutokomeza malaria kuwa ni Upuliziaji wa Viua Dudu katika mazalia ya
mbu,upatikanaji wa vyandarua kwa wajawazito na watoto wanaopata chanjo
ya surua / rubella, upatikanaji wa dawa ya SP kwa wajawazito kliniki,
vyandarua shuleni, upimaji wa vimelea vya malaria kwa wanaohisi kuwa na
homa kwa kutumnia mRDT`s na upatikanaji wa dawa mseto ya malaria.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi akihamasisha
jamii kuachana na imani potofu kuhusu matumizi ya vyandarua kwani baadhi
ya wanaume wamekuwa wakidai vyandarua vinapunguza nguvu za kiume.
Meneja Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T-
MARC, Hamid Al- Alawy akielezea namna wanavyoshirikiana na serikali ya
mkoa wa Shinyanga katika kupambana na malaria.
Meneja Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza
Malaria kutoka asasi ya T- MARC Tanzania, Hamid Al- Alawy alisema asasi
yake itatoa dawa na vifaa kusaidia kufanikisha zoezi la upuliziaji wa
viua dudu katika mazalia ya mbu kwenye halmashauri ya Ushetu.
Meneja Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T- MARC, Hamid Al- Alawy akizungumza ukumbini.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akiipongeza na
kuishukuru asasi ya T MARC Tanzania kwa kuendelea kushirikiana na
serikali katika mapambano dhidi ya malaria na kuwaomba kutekeleza mradi
wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria katika halmashauri ya Shinyanga
ambayo inashika nafasi ya pili kwa kuwa na kiwango kikubwa cha
maambukizi ya malaria baada ya Ushetu.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akihamasisha umuhimu
wa kushirikisha viongozi wa serikali za mitaa,viongozi wa
dini,mila,jeshi la jadi sungusungu kutoa elimu ya malaria na umuhimu wa
kupulizia dawa.
Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Daniel Mzee akitoa taarifa ya
hali ya malaria katika mkoa wa Shinyanga. Alisema halmashauri ya wilaya
ya Ushetu ikiongoza kwa kiwango cha asilimia 11.1% katika mkoa wa
Shinyanga. Dkt. Mzee alieleza kuwa dawa za kutibu malaria zinapatikana
katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya muda wote hivyo kuwaasa
wananchi kufika vituoni pindi waonapo dalili za malaria ili wapate
matibabu sahihi.
Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga,
Dkt. Daniel Mzee akitoa taarifa ya hali ya malaria katika mkoa wa
Shinyanga. Alisema vyandarua vyenye viuatilifu vinapatikana katika vituo
vyote kwa akina mama wajawazito wanaohudhuria kliniki kwa mara ya
kwanza na watoto wanaopata chanjo ya kwanza ya surua-rubella.
Wa kwanza kushoto ni Meneja Mradi wa
Badilisha Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T- MARC, Hamid Al-
Alawy akifuatiwa na Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Mohammed
Kahundi,Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume na Kaimu
Mkurugenzi Halmashauri ya Kahama Mji,Robert Kwela wakimsikiliza Mratibu
wa Malaria Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Daniel Mzee akitoa taarifa ya hali ya
malaria katika mkoa wa Shinyanga.
Wakurugenzi wa halmashauri za
wilaya,wajumbe wa timu ya usimamizi za afya mkoa na halmashauri,wadau wa
maendeleo na wahudumu wa afya ngazi ya jamii wakiwa ukumbini.
Mtoa huduma za afya Shema Lupiga
akielezea namna walivyonufaika na mafunzo kwa nadharia na vitendo kuhusu
namna ya kuendesha zoezi Upuliziaji wa Viua Dudu katika mazalia ya mbu.
Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya,wajumbe wa timu ya usimamizi za
afya mkoa na halmashauri,wadau wa maendeleo na wahudumu wa afya ngazi ya
jamii wakiwa ukumbini.
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Kahama Mji,Robert Kwela akizungumza ukumbini.
Wajumbe wa timu ya usimamizi za afya
mkoa na halmashauri, wahudumu wa afya ngazi ya jamii na wadau mbalimbali
wa afya wakiwa ukumbini.
Wajumbe wa timu ya usimamizi za afya
mkoa na halmashauri, wahudumu wa afya ngazi ya jamii na wadau mbalimbali
wa afya wakiwa ukumbini.
Wajumbe wa timu ya usimamizi za afya
mkoa na halmashauri, wahudumu wa afya ngazi ya jamii na wadau mbalimbali
wa afya wakiwa ukumbini.
Wajumbe wa timu ya usimamizi za afya
mkoa na halmashauri, wahudumu wa afya ngazi ya jamii na wadau mbalimbali
wa afya wakiwa ukumbini.
Wajumbe wa timu ya usimamizi za afya
mkoa na halmashauri, wahudumu wa afya ngazi ya jamii na wadau mbalimbali
wa afya wakiwa ukumbini.
Watoa huduma za afya waliopata mafunzo kuhusu namna ya kuendesha zoezi la Upuliziaji wa Viua Dudu katika mazalia ya mbu.
Uzinduzi huo umefanyika leo Jumamosi
Desemba 21,2019 katika bwawa la Shunu lililopo katika halmashauri ya Mji
Kahama na kuhudhuriwa na Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya,wajumbe
wa timu ya usimamizi za afya mkoa na halmashauri,wadau wa maendeleo
asasi ya T- MARC Tanzania na wahudumu wa afya ngazi ya jamii.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Upuliziaji wa Viua Dudu katika mazalia ya mbu ulioongozwa na kauli mbiu ya 'Ziro Malaria inaanza na mimi'
Kahundi alisema Viuadudu vinavyotumika kuweka katika madimbwi ya maji
havina madhara kwa watu na mifugo hivyo kuwataka wananchi wasiwe na
wasiwasi pale wanapoona wataalamu wa afya wakiweka viuadudu hivyo kwenye
madimbwi na mabwawa.
“Ushiriki wa jamii ni nguzo muhimu
katika kutokomeza malaria.Ili kufanikisha zoezi la upuliziaji wa
viuadudu ni lazima jamii ishirikishwe ili kuepuka mitazamo hasi kuhusu
zoezi hili. Shirikisheni Viongozi wa serikali za mitaa,vijiji na
kata,viongozi wa mila na dini na vikundi vya ngoma vinavyokubalika ili
kutokomeza malaria”,alisema Kahundi.
Kahundi alisema Maambukizi ya ugonjwa wa
malaria katika Mkoa wa Shinyanga ni asilimia 6.1 na kitaifa ni
asilimia 7.3 huku halmashauri ya wilaya ya Ushetu ikiongoza kwa kiwango
cha asilimia 11.1% katika mkoa wa Shinyanga.
“Hali ya kiwango cha maambukizi ya
malaria katika mkoa katika halmashauri ya Ushetu ni 11.1%, Shinyanga
6.9%,Msalala 6.2%,Kahama Mji 3.7%, Manispaa ya Shinyanga 3.1% na Kishapu
2.9%”,alisema Kahundi.
“Ugonjwa wa Malaria umekuwa ni
ugonjwa uliozoeleka, wananchi wamesahau kwamba ugonjwa wa malaria unaua
sana kwa muda mfupi mara tu usipopata matibabu kwa haraka, Malaria
hupunguza nguvu kazi, kupoteza rasilimali, mahudhurio hafifu mashuleni,
kupoteza maisha kwa wajawazito na kuharibika kwa mimba au kujifungua
kabla ya wakati”,alieleza Kahundi.
Alisema mkoa wa Shinyanga unaendelea
kupambana na ugonjwa wa malaria kwa njia mbalimbali ikwemo kuharibu
mazalio ya mbu, kutumia vyanadarua vyenye viuatilifu kuwapa elimu
wananchi elimu kuhusu malaria.
Akitoa taarifa ya hali ya Malaria katika
mkoa wa Shinyanga, Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Daniel
Mzee alisema lengo la zoezi la Upuliziaji wa Viua Dudu ‘Larviciding’
katika mazalia ya mbu ni kutekeleza agizo lililotolewa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu moja ya
mikakati ya kupambana na ugonjwa wa malaria nchini ili kutekeleza kauli
mbiu ya ‘Ziro Malaria inaanza na mimi’
Dkt. Mzee alisema jumla ya wahudumu wa
afya 35 kutoka kata zote za halmashauri ya Ushetu wamepatiwa mafunzo ya
namna ya kupulizia viua dudu kwa ufadhili wa asasi ya T- MARC Tanzania
wanaotekeleza mradi wa 'Badilisha Tabia Tokomeza Malaria' kwa ajili ya
kuhamasisha jamii kupambana na ugonjwa wa malaria katika halmashauri za
wilaya za Ushetu, Msalala na Kishapu.
Alieleza kuwa maambukizi ya malaria yanatokana na wananchi wengi
kutotumia vyandarua vyenye viuatilifu,elimu duni kuhusu malaria,usafi wa
mazingira na imani potofu juu ya matumizi ya vyandarua.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume
aliwakumbusha wakurugenzi wa halmashauri za wilaya kutenga fedha za
kutosha katika mipango ya halmashauri za kununulia dawa za viua dudu
ili zoezi la kupulizia viua dudu liwe endelevu katika halmashauri zote
za mkoa wa Shinyanga.
Naye Meneja Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T-
MARC Tanzania, Hamid Al- Alawy aliiomba serikali kuwatumia wahudumu wa
afya ngazi ya jamii waliopatiwa mafunzo na T -MARC Tanzania ili hata
watakapomaliza kutekeleza mradi wao wa 'Badilisha Tabia Tokomeza Malaria' kazi ya kupambana na malaria iwe endelevu.
“Wahudumu hawa wa afya tumewapa ujuzi na utaalamu wa kutosha.T MARC
inaahidi kutoa dawa na vifaa vya kuanzia katika zoezi la upuliziaji viua
dudu katika halmashauri ya Ushetu”,alisema Alawy.
Mmoja wa watoa huduma za afya waliopata mafunzo hayo, Shema
Lupiga alisema mafunzo hayo yalifanyika kwa nadharia na vitendo kuanzia
Desemba 18 hadi Desemba 21,2019 kuhusu namna ya kuendesha zoezi
Upuliziaji wa Viua Dudu katika mazalia ya mbu.
Aliyataja baadhi ya maeneo ya mazalia ya mbu ‘viluilui vya mbu’ kuwa ni mashamba ya mpunga,mabwawa,mashimo ya choo,makopo na madimbwi.
No comments :
Post a Comment