Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akiwa na Mtoto Anna
Zambi alipomtembelea nyumbani kwa mama yake Mdogo Mkoani Arusha Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu
akiwa na Mtoto Anna Zambi na mama mdogo yake Anna Bi. Isabella Lyimo
alipomtembelea nyumbani kwa mama yake Mdogo Mkoani Arusha.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
************************************
Na Mwandishi Wetu Arusha
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu leo
amtembelea mtoto Anna Zambi ambae alipoteza wazazi wake wote wawili na
wadogo zake
watatu katika ajali iliyotokea Korogwe Tanga, mwezi Octoba
2019.
Waziri Ummy
amemishi Mtoto Anna Zambi kujipa moyo na kujikaza na kumuomba Mungu
amsaidie kumpa faraja katika kipindi kigumu anachokipitia baada ya
kupotea wazazi wote na ndugu zake.
“Mimi nikutie
moyo mtoto wangu tuko pamoja na Serikali haitokuacha peke yako
tutajitaidi kukupa faraja kuwezesha kupata msaada wa huduma za msaada wa
kisaikolojia taratibu na kwa uweza wake Mungu utarudi katika hali yako
ya kawaida” alisema Mhe. Ummy
Kwa upande
mama yake mdogo mtoto Anna Bi. Isabella Lyimo wamemshukuru Mhe Ummy
kwa kumtembelea Anna na kuendelea kuwapa faraja.
Wazazi wa
Anna- Lingston Zambi na Winfrida Lyimo pamoja na ndugu zake watatu Lulu,
Adrew na Grace walifariki Dunia Oktoba 26 mwaka huu wakiwa njiani
kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Kilimanjaro, kwenye mahafali
ya Kidato cha Nne ya Anna, ambapo gari waliokua wakisafiria lilisombwa
na maji na mafuriko yaliyotokea wilayani Handeni mkoani Tanga.
No comments :
Post a Comment