Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)
akiwasilisha hoja ya Tanzania latina Mkutano wa 110 wa Baraza la
Mawaziri wa Nchi za Afrika,Carribean na Pacific (ACP) katika ushirikiano
na Jumuiya ya Ulaya unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano
wa Kenyatta (KICC) Nairobi, Kenya. Nyuma ya Prof. Kabudi ni Balozi wa
Tanzania Nchini Ubelgiji na Jumuiya ya Ulaya Balozi Jestas Nyamanga.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa
anajadili jambo na Balozi wa Tanzania Nchini Ubelgiji na katika Jumuiya
ya Ulaya Balozi Jestas Nyamanga (aliyesimama) akifuatiwa na Balozi wa
Tanzania Nchini Kenya Balozi Pindi Chana pamoja na baadhi ya maafisa wa
Ubalozi na wa Wizara ya Mambo ya NJe na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC) Nairobi Kenya.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa
anafuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri wa nchi za Afrika,Carribean
na Pacific (ACP). nyuma ya Prof. Kabudi ni Balozi wa Tanzania Nchini
Kenya Balozi Pindi Chana akifuatiwa na Balozi wa Tanzania Nchini
Ubelgiji na katika Jumuiya ya Ulaya Balozi Jestas Nyamanga.
***********************************
Tanzania imetoa
mapendekezo makuu matatu na yamekubaliwa katika kikao cha mashauriano
baina ya Mawaziri wa Baraza la Nchi za Afrika,Carribean na Pacific
kilichoanza
leo jijini Nairobi, Kenya.
Mapendekezo
hayo ya Tanzania yametolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Prof. Palamagamba John Kabudi katika Mkutano wa 110 wa Baraza
la mawaziri wa wa Nchi za Afrika,Carribean na Pacific katika ushirikiano
na Jumuiya ya Ulaya ambao utafuatiwa na Mkutano wa tisa wa wakuu wa
Nchi na Serikali katika jiji la Nairobi Nchini Kenya na kuongeza kuwa
Tanzania imetoa mapendekezo hayo ili kutodhoofisha umoja wa ACP hususani
katika kipindi hiki ambacho nchi hizo ziko katika majadiliano ya kina
na Jumuiya ya ulaya kuhusu mkataba mpya wa ushirikiano baada ya mkataba
wa sasa unaofikia ukomo Februari mwakani..
Ameitaja
sababu nyingine kuwa ni kuepuka mivutano isiyo na tija kati ya Nchi za
Afrika,Carribean na Pacific na Nchi za Jumuiya ya Ulaya hususani katika
nyakati ambazo nchi hizo zinahitaji mshikamano mkubwa zikiwa zinapita
katika kipindi muhimu cha kujenga uchumi na ustawi wa jamii ya nchi zao
na pia kujenga wigo wa kuaminiana baina ya Nchi wanachama.
Ameongeza
kuwa majadiliano baina ya Nchi wanachama wa ACP ni muhimu ili kupitia
upya mkataba wa George Town,mkataba ambao ndiyo ulianzisha Kundi la ACP
na kusainiwa katika jiji la Goergetown nchini Guyana mwaka 1975. Nchi za
ACP zimekubaliana kufanya mabadiliko makubwa ya Mkataba huo ili kujenga
Umoja wa ACP unaoendana na mabadiliko ambayo yamejitokeza ulimwenguni
na masuala mbalimbali ya Kimataifa ambayo yanahitaji mtazamo mpya.
Prof. Kabudi
amesema katika muktadha huo wa majadiliano, Tanzania imetoa mapendkezo
hayo matatu ambayo yote yamekubaliwa na kuungwa mkono na nchi zote 79
wananchama wa ACP jambo linaloonesha kuwa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania inaheshimika sana katika masuala ya kimataifa.
Akizungumzia
juu ya faida ya Mkutano huo wa Nchi za Afrika,Carribean na Pacific ,
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji ambaye pia anaiwakilisha Tanzania
katika Jumuiya ya Ulaya Balozi Jestas Abuok Nyamanga amesema kuwa
mkutano huo unatumika kama kutoa fursa kwa nchi 79 wanachama wa ACP
kutathmini changamoto mbalimbali zinazokabili nchi hizo, kuweka mikakati
ya pamoja na kuwa na sauti ya pamoja katika kusimamia utekelezaji wa
mikakati hiyo na katika majadiliano na Jumuiya ya Ulaya. Alisema kuwa
miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa na kuwekewa mikakati ya pamoja ni
pamoja na masuala yanayohusu uwekezaji, viwanda na biashara; uongezaji
wa mnyororo wa thamani katika mazao ya kilimo, kuongeza uwezo na wigo wa
ukusanyaji wa kodi. Mkutano huo pia unajadili namna ya kuwaongezea
uwezo wafanyabiashara wadogo,kuongeza ubunifu na matumizi sahihi ya
teknolojia na kukabiliana na mabadiliko ya tabiachi. Masuala yote hayo
ni moja ya kipaumbele cha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
katika awamu hii ya tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli.
Amehitimisha
kwa kusema katika mkutano huu Katibu Mkuu wa ACP anatarajiwa kuchaguliwa
ili kuweka mfumo mpya wa kiuongozi utakaosaidia wanachama wa ACP kupita
katika ushirikiano kwa miaka mingine ijayo katika ushirikiano baina ya
nchi za Afrika,Carribean na Pacific na Jumuiya ya Ulaya.
No comments :
Post a Comment