*****************************************
Kampeni ya Matibabu
ya Upasuaji wa Moyo Kwa watoto kutoka familia Duni iliyoanzishwa na Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda imezidi kuwa na mafanikio
makubwa ambapo Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania MOHAMED BIN
MANSOUR kupitia taasisi ya King Salman wameunga mkono jitiada hizo kwa
kumpatia madaktari bingwa wa Moyo ambao hadi siku ya leo wamefanya
upasuaji kwa Watoto 64 kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
RC Makonda
amemshukuru Balozi huyo kwa kuthamini uhai wa Watoto* hao ambao
waliteseka na kukata tamaa ya kuishi kutokana na Wazazi wao kushindwa
kumudu gharama za matibabu huku watoto wengine wakiwa ni yatima.
Aidha RC Makonda
amesema kuwa Kampeni ya kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni moja
kwaajili ya matibabu ya Moyo Kwa watoto zaidi ya 500 kutoka taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete inaendelea vizuri na hivi karibuni ataeleza hatua
iliyofikiwa.
Pamoja na hayo RC
Makonda amemuomba Balozi huyo wa Saudi Arabia na Mkurugenzi wa Taasisi
ya Moyo ya Jakaya kuangalia uwezekano wa Kupeleka kambi ya Matibabu ya
Moyo Mkoani Mwanza ili iweze kuwahudumia Wananchi wa Kanda ya Ziwa.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwetwe Prof. Mohammed Janabi
ameeleza kuwa upasuaji wa watoto hao 64 umeokoa kiasi cha Shilingi
Milioni 465 ambazo wazazi wangepaswa kutoa lakini kupitia diplomasia
nzuri kati ya Tanzania na Saudi Arabia watoto wao wamefanyiwa upasuaji
bure.
No comments :
Post a Comment