Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mzee
Zefania Kanoge Petro 82 ambaye anapatiwa matibabu katika hospitali ya
Wilaya ya Chato mkoani Geita. Mzee Kanoge ndiye aliyemshawishi Mhe.Rais
Dkt. Magufuli kuingia kwenye Siasa wakati alipokuwa akifanyakazi katika
Mkoa wa Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muungano ya Chato wakati wakati alipowakuta
katika Kiliniki wa Baba Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya
Chato wakisubiri kuchomwa Sindano za Chanjo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wazazi
waliowapeleka watoto wao kupewa chanjo katika Kliniki ya Baba Mama na
Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Chato.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi
mbalimbali pamoja na Madaktari wa Hospitali hiyo ya Chato mara baada ya
kuwajulia hali wagonjwa pamoja na kutembelea Kliniki ya Watoto
hospitalini hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wafiwa
katika msiba wa mzee Mariganya Ng’wenge aliyefariki tarehe 4/11/2019 na
anatarajiwa kuzikwa kesho Choto mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwanunulia madaftari
wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato Ladislaus , Daudi Petro na Shemila
Mlegete mara baada ya kukutana nao katika eneo la Chato mjini wakati
wakitokea shuleni kwao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika kaburi la
Shangazi yake Salome Michael Nyahinga katika eneo la Chato wakati
akitokea kuhani Msiba wa Mzee Mariganya Nghwenge katika eneo la Ginnery
Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mkazi wa Chato
Venance Magege wakati aliposimama kuwasalimia wananchi wa Chato mjini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi wa
Chato mjini mara baada ya kusimama kuwasalimia wakati akitokea kuhani
msiba wa mzee Mariganya Ng’wenge katika eneo la Ginnery Chato mkoani
Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na
wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato Shemla Mlegete wakwanza kushoto,
Ladislaus katikati pamoja na Daudi Petro mara baada ya kuwaona wakati
akitoka akizungumza na wananchi wa Chato.
Picha ya Kumbukumbu- Marehemu mzee
Mariganya Nghwenge aliyefariki juzi akiwa ameshikilia Mhogo mrefu
alipokuwa akimuonesha Rais wa kwanza wa Tanzania Baba wa Taifa Hayati
Mwalimu Julius Nyerere (haonekani pichani) mwaka 1967 katika eneo la
Ginnery Chato mkoani Geita. Mzee huyo alikuwa akionesha namna gani
alikuwa Mkulima bora katika kipindi hicho. PICHA NA IKULU
No comments :
Post a Comment