Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Ally Possi akitoa maelekezo kwa
uongozi wa Chama cha Maafisa Habari Tanzania (TAGCO) wa kuendeleza
mpango wa kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa maafisa habari wa
serikalini leo alipokuwa akifunga mafunzo ya maafisa hao yaliyokuwa
yakifanyika jijini Dodoma kwa siku tano.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Ally Possi akimkabidhi cheti
Afisa Habari kutoka Ofisi ya Rais Utumishi Menejimenti na Utawala Bora
Bibi.Happy Shayo katika sherehe ya kufunga Mafunzo ya Maafisa Habari
Serikalini leo yaliyokuwa yakifanyika Jijini Dodoma kwa siku tano ambayo
yaliandaliwa na uongozi wa chama cha maafisa habari Tanzania (TAGCO).
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Ally Possi (aliyeketi watatu
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Habari kutoka
Ofisi za Mikoa na Serikali za Mitaa baada ya kufunga mafunzo ya Maafisa
Habari Serikalini yaliyokuwa yakifanyika Jijini Dodoma kwa siku tano,wa
kwanza kulia ni Katibu wa Chama cha Maafisa Habari Serikalini Tanzania
(TAGCO).
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Ally Possi akionyesha Jarida la
Nchi Yetu linaloandaliwa na Idara ya Habari MAELEZO, lililo sheheni
taarifa mbalimbali za utekelezaji wa serikali ya awamu ya tano kwa miaka
minne maara baada ya kukabidhiwa jarida hilo katika sherehe za kufunga
mafunzo ya Maafisa Habari Serikalini yaliyokuwa yakifanyika Jijini
Dodoma kwa siku tano.
………………
Na Shamimu Nyaki – WHUSM,Dodoma
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi amewapongeza Maafisa
Habari,Uhusiano na Mawasiliano Serikalini kwa kutangaza vizuri
shuguli
za Serikali ikiwemo miradi inayotekeleza ambayo itawaletea wananchi
maendeleo.
Dkt.Possi ameyasema hayo leo
Jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo ya kimkakati ya Uandishi wa Habari
za Serikali ya awamu ya pili kwa Maafisa Habari,Uhusiano na
Mawasiliano Serikalini ambapo amewataka kutumia elimu waliyopata
kuendelea kuhabarisha umma kwa weledi na kwa usahihi habari zinazohusu
Serikali.
“Maafisa Habari mnafanya vizuri
katika kutangaza shughuli za Serikali kwa wananchi,naomba muendelee
kufanya hivyo kwa kuwa kada yenu ni muhimu katika kufikisha ujumbe wa
Serikali kwa wanachi na mtumie kalamu zenu vizuri ili kulinda na
kudumisha amani ya nchi yetu”alisema Dkt. Possi.
Aidha Dkt.Possi amewataka
waandaaji wa mafunzo hayo kuendelea kutoa mafunzo hayo mara kwa mara kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali pamoja na kutumia mifumo tofauti ya
ndani na nje ya nchi pamoja na kufanya tathmini ili kuona mabadiliko
yaliyopatikana kutokana na mafunzo hayo.
Hata hivyo Dkt. Possi aliwashauri
Maafisa Habari wote wa Serikali kujiunga na Chama cha Maafisa
Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) ili kurahisisha mawasiliano miongoni
mwao pamoja na kushirikiana katika kazi wanazofanya ikiwemo
kubadilishana uzoefu na kusaidiana kijamii na kitaaluma.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Habari –MAELEZO Bw.Rodney Thadeusi amesema kuwa
jukumu la maafisa habari wa Serikali ni kutoa taarifa sahihi na kwa
wakati zinazohuzu Serikali kwa wananchi kutumia njia zote za mawasilano .
“Maafisa habari kazi yetu kubwa ni
kuisemea Serikali tusiposema sisi wengine watasema na wengine wanaweza
kusema ambayo sio sahihi na wakati mwingine kukosoa hata yale mazuri
ambayo Serikali inatekeleza kwa wananchi wake hivyo tuendelee kutumia
taaluma yetu kuitangaza vizuri Serikali”alisema Bw.Rodney.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama
hicho Bibi.Sara Msika amesema lengo la mafunzo hayo ni kuendelea
kuboresha taaluma ya maafisa hao katika kipindi hiki ambacho dunia
imekuwa na mabadiliko makubwa katika kada hii ya uandishi wa habari .
Mmoja wa washiriki wa mafunzo
hayo Afisa Habari kutoka TBC Bibi.Catherine Nyoni ameshukuru waandaaji
wa mafunzo hayo kwa kuona umuhimu wa kutoa mafunzo kwa Maafisa Habari
Serikalini ambayo yamesaidia kuboresha taaluma yao pamoja na
kubadilishana uzoefu.
Mafunzo hayo ya siku tano
yalioandaliwa na Idara ya Habari –MAELEZO pamoja na Chama cha Maafisa
Mawasiliano Serikalini (TAGCO) yamekuwa na mada mbalimbali ikwemo namna
ya kutumia mitandao ya kijamii kuhabarisha umma pamoja na uandishi mzuri
wa habari za Serikali.
No comments :
Post a Comment