Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa Na Michezo Juliana Shonza akipokea tuzo kwa niaba ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Desemba 5, 2019
katika ukumbi wa Karimjee uliopo jijini Dar es salaam aliyotunukiwa na
Shirika lisilo la Kiserikali la Kuinua Diplomasia ya Uchumi Tanzania
(TEDEF) kwa kuwa mstari wa mbele kuinua diplomasia ya uchumi nchini.
aibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa Na Michezo Juliana Shonza akihutubia hadhira iliyohudhuria hafla
ya kukabidhi tuzo kwa Watanzania 10 waliofanya vizuri kwa kutoa mchango
wao katika kuimarisha Diplomasia ya Uchumi wa nchini iliyofanyika
Desemba 5, 2019 katika ukumbi wa Karimjee uliopo jijini Dar es salaam
Octavian Kimario kutoka Wazara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa Na Michezo akipokea tuzo kwa niaba ya Mchezaji
wa Kimataifa Mbwana Samata wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa
Watanzania 10 waliofanya vizuri kwa kutoa mchango wao katika kuimarisha
Diplomasia ya Uchumi wa nchini iliyofanyika Desemba 5, 2019 katika
ukumbi wa Karimjee uliopo jijini Dar es salaam
Mwimbaji Rahabu Matitu akiwa na
kwayainayojulikana kwa jina la Mshumaa Group ya Sinza E jijini Dar es
salaam wakitumbuiza wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa Watanzania 10
waliofanya vizuri kwa kutoa mchango wao katika kuimarisha Diplomasia ya
Uchumi wa nchini iliyofanyika Desemba 5, 2019 katika ukumbi wa Karimjee
uliopo jijini Dar es salaam
(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dar es Salaam)
……………………..
Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dar es Salaam
Shirika lisilo la Kiserikali la
Kuinua Diplomasia ya Uchumi Tanzania (TEDEF) limetambua
juhudi na
kuthamini kazi anazofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt.
John Pombe Magufuli kuhakikisha azma ya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa
kati ifikapo 2025 inafikiwa.
TEDEF imemtunuku tuzo Rais Dkt.
Magufuli na kuwa miongoni mwa Watanzania 10 waliofanya vizuri kwa kutoa
mchango wao katika kuimarisha Diplomasia ya Uchumi wa nchini.
Akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya
Rais Dkt. Magufuli na kuwakabidhi tuzo hizo watanzania wengine
waliomstari wa mbele kuinua diplomasia ya uchumi nchini Desemba 5, 2019
katika ukumbi wa Karimjee uliopo jijini Dar es salaam, Naibu Waziri Wa
Habari, Utamaduni, Sanaa Na Michezo Juliana Shonza ameishukuru TEDEF kwa
uamuzi wao wa kushirikiana na Serikali katika kuimarisha diplomasia ya
Uchumi nchini.
“Diplomasia ya Uchumi ni Muhimu
kwa ustawi wa Taifa. Mataifa yote makubwa duniani yameupa umuhimu wa
kwanza Diplomasia ya Uchumi ambao umekuwa ni muhimili wa kukuza mataifa
hayo. Nanyi TEDEF mmekuwa wazalendo kwa kutambua na kuthamini mchango wa
viongozi na wananchi mbalimbali katika kuhakikisha nchi yetu inafikia
azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati” alisema Naibu Waziri Shonza.
Miongoni mwa kazi zilizomfanya
Rais Dkt. Magufuli kupewa tuzo hiyo mchango wake katika kujenga
miundombinu ya kufanikisha Diplomasia ya Uchumi Tanzania ikiwemo miradi
ya reli ya kisasa (SGR), kuimarisha shirika la ndege, ujenzi wa
barabara na madaraja mbalimbali nchini pamoja na Mradi wa umeme Bwawa
la Nyerere.
Watanzania wengine waliopata tuzo
za kushiriki kujenga diplomasia ya uchumi ni mawaziri wawili ambao ni
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.
Palamagamba Kabudi kwa kuongoza majadiliano ya Biashara ya Kimataifa
baina ya Tanzania na Kampuni ya Madini ya Barrick kwa mafanikio makubwa
kwa Tanzania pamoja na Wiziri wa Mambo ya Ndani nchi Kangi Lugora ambaye
anasimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao kwa kutambua amani
iliyojengeka ni muhimu kwa kufanikisha Diplomasia ya Biashara na
Diplomasia ya Uchumi.
Tuzo hizo pia zimeenda kwa
Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi ambao nao wametambuliwa
kwa mchano wao katika kujenga diplomasia ya uchumi; Ubalozi wa Tanzania
Nchini Rwanda ukiongozwa na Balozi Ernest Mangu ambao umeongoza kwa
mauzo ya nje katika nchi za Afrika Mashariki, Ubalozi wa Tanzania nchini
China ukiongozwa na Balozi Mbelwa Kairuki kwa kwa kuongoza katika
uwekezaji mitaji nchini pamoja na Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani
ukiongozwa na Balozi Wilson Masilingi ambao umeongoza kwa kuleta watalii
nchini.
Mbali na viongozi hao, Mkoa wa Dar
es Salaam ambao unaongozwa na Mkuu wa mkoa huo Paul Makonda nao umepata
tuzo hiyo kwa kuongoza kwa miradi ya uwekezaji ambapo takribani miradi
109 imesajiliwa.
Aidha, Watanzania wengine ambao
wametambuliwa kwa mchango wao katika kushiriki katika kuitangaza
Tanzania kimataifa katika diplomasia ya uchumi na kupewa tuzo hiyo ni
mchezaji wa mpira wa miguu Mbwana Samata kupitia sekta ya michezo,
mwanamuziki Nasibu Abdul (Diamond) kupitia sekta ya muziki pamoja na
mtangazaji wa TBC Elisha Elia anayetangaza kipindi cha Kishindo cha
Awamu ya Tano na kusaidia kutangaza miundombinu ya Diplomasia ya
Biashara na Diplomasia ya Uchumi kupitia sekta ya habari.
Kwa upande wake Mkurugenzi na
Makamu Mwenyekiti Bodi ya TADEF Dkt. Wilbroad Mtabuzi ameyataja baadhi
ya majukumu ya msingi ya shirika hilo kuwa ni pamoja na kuvutia
uwekezaji hasa kwenye viwanda, Kuhamasisha biashara ya kimataifa
kuhamasisha utalii, kutangaza sifa njema za nchi yetu ambayo ni amani,
utulivu na umoja wa Kitaifa ambapo majukumu hayo yatasaidia kuchangia
kasi yakuufikia uchumi wa kati.
Dkt. Mutabuzi amesema kuwa TEDEF
imefanikiwa kuunda vyama vya ushirika kwa wahimitimu wa elimu ya juu
nchini ambao wamejiajiri katika katika sekta ya kilimo-biashara kwenye
mikoa ya mikoa ya Dare es salaam, Pwani, Dodoma, Kigoma, Mbeya na
Mwanza.
Wahitimu hao wamefanikiwa
kuanzisha vikundi vya ufugaji samaki kibiashara katika mkoa wa Pwani
eneo la Ruvu wilayani Bagamoyo pamoja na kuwasaidia wakulima zaidi ya
2000 wanaojishughulisha na kilimo wamenufaika na huduma za TEDEF nchini.
Sera ya Diplomasia ya Uchumi Mwaka
2001 nchini ilianza kutekeleza kufuatia idhini ya Rais wa Awamu ya Tatu
Benjamin William Mkapa mwaka 2000 ikitambua kuwa Diplomasia ya Uchumi
ni Ustawi ambapo ushiriki wa TEDEF katika diplomasia hiyo una mchango
katika kuleta ustawi katika nchini.
No comments :
Post a Comment