Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani ( mwenye shati la bluu) akiwasili kwenye ufunguzi wa kiwanda
cha Nguzo cha Qwihaya kilichopo wilayani Kasulu.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard
Kalemani, akipata maelekezo kuhusu kiwanda cha Qwihaya kutoka kwa mmoja
wa mfanyakazi wa kiwanda hicho.
Mmoja wa mtambo inayotumika kuzalishia nguzo za umeme katika kiwanda cha Qwihaya kilichopo wilayani Kasulu.
Nguzo za umeme zinazozalishwa na kiwanda cha Qwihaya zikiwa tayari kwaajili ya matumizi.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kiwanda cha nguzo cha Qwihaya.
Waziri wa Nishati, Dkt Kalemani
akimpongeza Leonard Mahenda ambae ndio mmiliki wa kiwanda cha Qwihaya
mara baada ya kukata utepe.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard
Kalemani( wa kwanza kulia), Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako na Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga
wakiwa kwenye ufunguzi wa kiwanda cha Nguzo za Umeme cha Qwihaya.
……………..
Hafsa Omar-Kigoma
Waziri wa
Nishati, Dkt Medard Kalemani, amefungua kiwanda cha Nguzo cha Qwihaya,
kilichopo katika Mtaa wa Kasanga, Wilaya ya Kasulu, Mkoani Kigoma
Akizungumza
kwenye mkutano wa hadhara, mara baada ya ufunguzi wa
kiwanda hicho Dkt.
Kalemani alieleza kuwa Serikali ilikuwa inapata gharama kubwa kutoa
Nguzo katika Mikoa mengine kuzifikisha Mkoani humo kabla ya kiwanda
hicho kujengwa Mkoani humo.
Alisema, maeneo
ambayo yapo karibu na kiwanda hicho yatafikiwa na umeme kwa haraka
kwasababu hakutakuwa na sababu ya ucheleweshaji wa kupeleka umeme katika
maeneo hayo ambayo, kiwanda cha nguzo kipo karibu.
Aliongeza kuwa,
Serikali haitakubali kuona ucheleweshwaji wa usambazaji umeme
vijijini, kupitia TANESCO au Wakandarasi, kwasababu ya uwepo wa
kiwanda hicho Mkoani humo umewarahisishia kazi na bei ya nguzo itashuka
ikilinganishwa na bei ya Nguzo ambazo zinatoka katika Mikoa ya Njombe
na Iringa.
“ Maelekezo yangu
kwa TANESCO ni kuanza kuzichukua nguzo hizi kwa njia ya ushindani
hakuna tena sababu ya kusema nguzo hakuna na nataka kazi zimalizike
ndani ya muda kwasabau vitendea kazi vipo na pesa ipo” alisema.
Alifafanua kuwa,
mahitaji ya nguzo kwa sasa nchini ni milioni moja na nusu kwa mwaka
lakini wazalishaji nchini wanauwezo wa kuzalisha zaidi ya nguzo milioni
tatu ukilinganisha na mwaka 2015 ambapo mahitaji ya nguzo yalikuwa
milioni moja na nusu lakini nguzo zilizokuwa zinapatikana nchini ni laki
nne tu, ambapo nguzo nyingi zilikuwa zinatoka Nchi za nje lakini kwa
uwepo wa viwanda nchini imesaidia sana upatikanaji wa nguzo kwa wingi.
Alieleza kuwa,
kwa kipindi cha miaka minne viwanda vya nguzo tisa vimejengwa nchini,
mara baada ya Serikali kupiga marufuku ya ununuaji nguzo kutoka nchi za
nje ambao ulikuwa unachelewesha usambazaji wa umeme nchini .
Aidha,
alimpongeza muwekezaji wa kiwanda hicho, kwa kujitolea kujenga kiwanda
kwenye eneo hilo pamoja na kumiliki viwanda vyengine Mkoani Njombe na
Iringa na kuamua kuwekeza katika maeneo mengine ya nchini.
Kwa kuona umuhimu
wa Viwanda hivyo, Waziri Kalemani ametoa wito kwa wawekezaji wengine
wajitokeze kujenga viwanda vya Nguzo, katika Mikoa mengine nje ya Mkoa
wa Iringa na Njombe ili kutimiza azma ya Rais ya Tanzania ya Viwanda.
Awali, Kaimu
Mkurugenzi wa kiwanda hicho Beruto Kaboda ameleza kuwa kiwanda chao
kimeamua kimeitikia wito wa Rais, wa Tanzania ya Viwanda kwa vitendo kwa
kuchukua hatua ya kujenga kiwanda hicho chenye uwezo wa kuzalisha
zaidi ya nguzo laki moja kwa mwaka.
Vile vile,
alieleza kuwa kwasasa soko lao kubwa lipo hapa nchini na mteja wako
mkubwa ni Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO) ambapo kipindi hiki cha
utekelezaji wa mradi wa REA awamu ya tatu soko la nguzo limekuwa
kubwa na kuwalazimu kufanya kazi kwa masaa 24.
Pia alitoa
shukrani zake kwa Waziri wa Nishati Dr Medard Kalemani na Naibu Waziri
Subira Mgalu kwa kuwasimamia wazalishaji wa nguzo nchini na kutoa
miongozo ambayo inawapa hamasa ya kufanya kwa bidii na kuhakikisha
wanazalisha nguzo bora na zinawafikia wananchi wa vijiji kwa haraka
zaidi.
No comments :
Post a Comment