Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Menejimenti ya
Shirika la Nyumba la Taifa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam
alipokutana kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa Shirika hilo.
Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC Dkt Maulid Banyani.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na
Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) alipokutana nayo
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kujadili uboreshaji wa Shirika
hilo. Kulia aliyekaa ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC Dkt Maulid Banyani
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa maelekezo kwa Kaimu
Mkurugenzi wa Ubunifu wa NHC Margreth Ezekiel (Kulia) na Mhandisi
Mburuga Matamwe wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Machinjio ya
Vingunguti mwishoni mwa wiki. 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipata maelezo kutoka kwa Kaimu
Mkurugenzi wa Ubunifu wa NHC Margreth Ezekiel wakati akikagua maendeleo
ya ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti mwishoni mwa wiki. Wa Kwanza
kushoto ni Mhandisi kutoka NHC Mburuga Matamwe.
(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
********************************
Na Munir Shemweta WANMM
Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amekutana na
Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa saa nne na kulitaka
shirika hilo kuhakikisha kufikia Januari 2020 inawachukulia hatua
wapangaji wote wa Shirika hilo wanaodaiwa kodi inayofikia bilioni 8.23.
Dkt Mabula
alikutana na Menejiment ya Shirika hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es
salaam ikiwa ni mkakati wake wa kulifanya Shirika la Nyumba la Taifa
kuimarika kimapato pamoja na kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Alisema, katika
kuifanya NHC inaimarika kimapato ni lazima madeni kutoka kwa wapangaji
wake yanakusanywa kwa kuanzisha opreresheni maalum inatakayowezesha
kutambuliwa wadaiwa wote wa kodi ili waweze kulipa kwa wakati.
‘’Ukiacha zile
taasisi za serikali, wote wanaodaiwa ikifika januari 2020 wafikishwe
kwenye vyombo vya sheria na zile taasisi za serikali mkamuone Katibu
Mkuu HAZINA ili taasisi hizo zikatwe fedha moja kwa moja’’ alisema Dkt
Mabula
Kwa mujibu wa
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, wakati wa zoezi la
kufanya opresheni ya kukusanya madeni sheria lazima ifuatwe ikiwemo
kutoa hati za wito wa madai kwa wadaiwa wote kabla ya hatua nyingine
kuchukuliwa.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Umiliki na Uendelezaji wa Shirika la Nyumba la Taifa
Greyson Godfrey alimueleza Dkt Mabula kuwa, pamoja na NHC kuimarika
katika makusanyo lakini liko kwenye mikakati maalum wa kukusanya madeni
kutoka kwa wadaiwa wake na moja ya jitihada zake ni kuingia makubaliano
maalum ya namna wadaiwa watakavyolipa madeni.
Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Nyumba la Taifa Dkt Maulid Banyani alisema Shirika lake
limekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha linaimarika kimapato
ikiwemo kutoa motisha kwa watumishi wanaofanya vizuri katika mikoa
itakayofikia lengo la makusanyo na kutokuwa na malimbikizo ya madeni
kutoka kwa wadaiwa wa kodi.
‘’Tumekuwa
tukitoa motisha kwa watumishi wanaofanya vizuri na sasa tunaangalia ile
mikao ambayo haina malimbikizo ya madeni kwa wapangaji wake kwa asilimia
mia moja tuone namna tutakavyotoa motisha ili kuhamasisha mikoa
kutokuwa na madeni’’ alisema Dkt Banyani
Aidha, Dkt
Banyani alisema, kwa sasa NHC imeanza kufanya uhakiki kwa wapangaji wake
ili kubaini wapangaji waliopangisha watu wengine ambapo eneo la Ubungo
limetumika kama eneo la majaribio na tayari wapangaji sita
washaondolewa na kusisitiza kuwa zoezi hilo litakuwa ni la nchi nzima.
Katika hatua
nyingine Naibu Waziri Mabula aliagiza kupatiwa orodha ya nyumba zote za
NHC zilizouzwa, zisizouzwa, zilizopangishwa na zisizozopangishwa,
viwanja vya Shirika hilo visivyoendelezwa pamoja na Nyumba zilizokuwa za
Msajili wa Majumba zilizohamishiwa NHC hilo ili kujua hali ya shirika
na mkakati wake katika kuleta ufanisi.
Pia Dkt Mabula
alitembelea maendeleo ya ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti na
kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo ambao uko katika hatua za mwisho
za kukamilika.
No comments :
Post a Comment