NA
VERONICA MWAFISI, MOHA
WIZARA
ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, kesho Desemba
3, 2019, itafanya uzinduzi wa kuhuisha takwimu za wakimbizi waishio jijini Dar
es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Huduma kwa Wakimbizi katika Wizara hiyo imefafanua kuwa, uhakiki huo utafanywa na idara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR).
“Uhuishaji
takwimu utahusisha wakimbizi wote waishio Dar es Salaam wenye nyaraka,
walioruhusiwa kuishi nje ya kambi za wakimbizi na maeneo mengine kuanzia saa 2
asubuhi,” ilifafanua taarifa hiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, baada ya uzinduzi uhuishaji takwimu utafanyika katika
Ofisi za Shirika la Relief of Development Society (REDOSO).
Ofisi
hizo zipo Kinondoni, Biafra ambapo wakazi, waombaji hifadhi wote pamoja na
familia zao, wanapaswa kufika ili kuhuisha takwimu zao bila kukosa.
Mkimbizi
yeyote ambaye hatajitokeza wakati wote wa uhuishaji takwimu taarifa zake
hazitahuishwa na usajili wake utasitishwa.
Wakimbizi
hao wametakiwa kufika na nyaraka za utambulisho zikiwemo barua ya uthibitisho wa
mkimbizi, usajili, kibali cha kuishi nje ya kambi, vyeti vya kuzaliwa.
Nyaraka
nyingine ni vyeti vya ndoa, hati ya kusafiria, vitambulisho vya kazi, shule,
chuo na nyaraka nyingine yoyote inayomtambulisha mkimbizi ambayo inatambulika
kisheria.
“Shughuli
zote zinazohusiana na uhakiki wa taarifa za mkimbizi na waomba hifadhi zinatolewa
bure.
No comments :
Post a Comment