Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi kutoka Burundi, Pascal Barandagiye (kushoto) na Kamishna Msaidizi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), George Okoth
Obbo wakibadilishana mkataba unaohusu makubaliano ya pande hizo
tatu katika kuhakikisha urejeshwaji wa wakimbizi wa Burundi
wanaotaka kurejea nchini kwao kwa hiari.
Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akisaini
moja ya mkataba unaohusu makubaliano katika kuhakikisha
urejeshwaji wa wakimbizi wa Burundi wanaotaka
kurejea nchini kwao kwa hiari.Wanaoshuhudia ni
Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi,Sudi Mwakibasi na Katibu Tawala
Mkoa wa Kigoma,Rashid Mchata. Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi kutoka Burundi, Pascal Barandagiye, akisaini moja ya mkataba unaohusu
makubaliano katika kuhakikisha urejeshwaji wa wakimbizi wa
Burundi wanaotaka kurejea nchini kwao kwa hiari.
Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), George Okoth
Obbo, akizungumza wakati wa Kikao cha makubaliano katika kuhakikisha
urejeshwaji wa wakimbizi wa Burundi wanaotaka
kurejea nchini kwao kwa hiari. Kulia ni
Mwakilishi wa UNHCR nchini Tanzania,Chansa Kapaya.Tukio hilo limefanyika jijini
Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,
Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akizungumza wakati wa Kikao
cha makubaliano katika kuhakikisha urejeshwaji wa wakimbizi
wa Burundi wanaotaka kurejea nchini kwao
kwa hiari.Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI).NA ABUBAKARI AKIDA, MOHA
SERIKALI ya Tanzania imepinga tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba imekua
ikiwafukuza wakimbizi kutoka nchini Burundi wanaoishi katika makazi na kambi
mbalimbali katika mikoa ya Kigoma,Tabora na Katavi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Kangi Lugola katika
kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam kikihusisha pande tatu;Serikali ya
Tanzania,Serikali ya Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia
Wakimbizi(UNHCR),huku mkataba maalumu ukisainiwa na pande hizo tatu lengo ni
kuwezesha urejeshwaji wa wakimbizi walioomba kurejea nchini kwao baada ya amani
kurejea.
“Ni vyema tukaliweka hili wazi ili jumuiya za kimataifa na Mataifa mengine
yajue kwamba tunaposema tunawarejesha wakimbizi wa Burundi sisi na Serikali ya
Burundi tunachofanya ni kuhamasisha,kuhimiza wale ambao wako na hiari warudi
Burundi,baada ya kugundua amani imerejea Burundi,sasa tunapofanya hivyo wenzetu
wanatafasiri kwamba tunawafukuza wakimbizi,hiyo sio sahihi,serikali ya Tanzania
na wananchi wake kwa ujumla wamekua wakipokea wakimbizi kutoka nchi mbalimbali
na hatujaanza leo tumekua tukiwahifadhi na amani inaporejea wanaomba warejee
katika nchi zao” alisema Lugola
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Mambo ya Ndani kutoka nchini
Burundi,Pascal Barandagiye amesemaBurundi sasa ina amani na wameona ipo haja ya
raia wake warejee ili kuweza kuijenga nchi yao.
“Tunawahakikishia kwamba kama nchi tuna uwezo wa kupokea warundi 2000 kwa
wiki na sisi tutahakikisha warundi wote wanarejea nyumbani,tutawafuata popote
walipo,tunawahitaji warudi nyumbani ili tuje tujenge nchi yetu pamoja,” alisema
Barandagiye
Kwa upande wa Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Kuhudumia wakimbizi(UNHCR),George Okoth Obbo alisema wameshirikiana na nchi
mbili za Tanzania na Burundi katika kuhakikisha yanakuwepo mazingira salama na
yenye utu katika uendeshaji wa zoezi hilo huku akiwashukuru Watanzania kwa
mwema wao wa kuendelea kuwapokea wakimbizi.
“Tanzania imekua nchi rafiki kwa wakimbizi,mawaziri wote wawili
wamekubaliana suala la kurudi wa warundi nchini kwao,tuko hapa kuhakikisha
zoezi hilo litaenda salama likizingatia ustawi wa pande zote tatu” alisema
Okoth
Ni takribani mwezi mmoja umepita tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt.John Magufuli kwenye ziara yake katika mkoa wa Katavi kuagiza
pande zote zinazohusiana na masuala ya wakimbizi wakutane ili kuweza kujadili
suala la warundi wanaojiandikisha kwa hiari kurudi nchini kwao,akiwaambia
umefika wakati sasa wakurudi katika nchi zao kwenda kuzijenga huku
akiwaonya wakimbizi wanaoshiriki katika matukio ya uhalifu hapa nchini.
No comments :
Post a Comment