Cheti cha Top Employer Award in Tanzania ambacho kampuni imetunukiwa

Wafanyakazi wa TBL wakifurahia Tuzo ya Kampuni muda mfupi baada ya kukabidhiwa
………………..
Taasisi ya
kimataifa ya masuala ya Raslimali Watu na ajira ijulikanayo kama Top
Employer Institute, yenye Makao yake makuu nchini Uholanzi imeitunukia
tuzo ya Mwajiri Bora 2019 kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL),
kutokana na kuzingatia na kutekeleza
kanuni za Raslimali Watu na uajiri
ipasavyo ikiwa ni ushindi wa mwaka wa tatu mfululizo ambapo mwaka juzi
na mwaka jana pia ilishinda tuzo hiyo.
Vigezo vya ushindi
vimetokana na utafiti wa taasisi ya Top Employers kwa makampuni
mbalimbali makubwa nchini ambao ulilenga kwenye utekelezaji kanuni za
ajira na Raslimali watu, kampuni ya TBL, imebainika kuwa na vigezo vya
ubora katika utekelezaji wa kanuni za ajira zinavyotakiwa.
Baadhi ya vigezo
ambavyo vilifuatiliwa katika utafiti huo kutoka kwa waajiri ni mikakati
ya kukuza vipaji vya wafanyakazi, mpangilio wa kazi wa kila siku,
mazingira ya kazi, uendelezaji wafanyakazi kimafunzo, utawala sehemu za
kazi, taaluma na upandishaji wa vyeo kwa wafanyakazi, maslahi ya
wafanyakazi na malipo ya stahiki zao kwa ujumla na desturi ya kampuni.
Mkurugenzi Mkuu wa
TBL, Philip Redman alisema “Kampuni yetu inajivunia kupata tuzo hii
kwa kipindi cha miaka 3 mfululizo, hii inadhihirisha mwendelezo wa
dhamira yetu wa kuifanya kampuni yetu mwajiri bora anayekidhi viwango
vya ndani na vya kimataifa,”
TBL, mbali na
kushinda tuzo hii ya uajiri bora ngazi ya kimataifa pia inashikilia
rekodi ya kuwa mwajiri bora nchini ambapo mwaka 2015 na 2016 ilishinda
tuzo ya Mwajiri Bora inayotolewa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE).
“Tunajivunia kwa mafanikio ya kampuni inayoendelea kuyapata na tutazidi
kuboresha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wetu kwa kuwa ni moja ya
sera yetu”. Alisema Redman.
TBL, ilitangazwa rasmi kuwa mshindi wa tuzo hii katika hafla iliyofanyika Johanesburg nchini Afrika ya Kusini hivi karibuni.
No comments :
Post a Comment